Saturday, July 15, 2017

Polepole ziarani Pwani: Akemea vikali wanaokiuka katiba na kanuni za uchaguzi






Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa itikadi na uenezi ndugu Humphrey Polepole leo tarehe 15/07/2017  amehudhuria mahafali ya Umoja wa Vijana wa CCM vyuo na vyuo vikuu mkoa wa pwani,wilaya ya Bagamoyo katika ukumbi wa Mageti mia na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama wilaya na mkoa.

Baadhi ya viongozi hao ni Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Ndg Anastazia Amasi, mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Ndg Shukuru Kawambwa, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ndg Ridhiwan Kikwete na viongozi wa wilaya.

Ndugu Mwenezi taifa amehudhuria Sherehe hizo baada ya Vijana wa vyuo na vyuo vikuu Umoja wa Vijana wa CCM kumwalika katika  tukio hilo la kuwaaga vijana wa  CCM wanavyuo kwa ajili ya kuhitimu masomo yao.

Ndugu Humphrey Polepole ambaye alikuwa mgeni rasmi awali alipata heshima ya kupokelewa na wazee wa Bagamoyo na kusomewa dua maalum na kumkabidhi zawadi za kumpongeza kwa kazi nzuri na kubwa anayoifanya kwa nchi na chama.

Ndg Polepole baada ya kupata Dua na taarifa fupi kutoka kwa uongozi wa CCM  mkoa  alienda kuhuduria mahafali ya wanavyuo mkoa wa pwani ndipo alipata wasaa wa kuwausia na kuwasisitiza wanavyuo kuhusu kusoma, kuishi na jamii vizuri watakapo maliza masomo yao, kuheshimu wazee, kujituma na kuwa wazalendo.

Ndg Mwenezi alitoa tahadhari na onyo kwa wote waliochukua Fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama na alisema kuhusu wanachama wa CCM wa ngazi zote walioomba uongozi ndani ya chama na  wanavyeo vingine.
Ndugu Polepole alisema;

"Tumekubaliana cheo kimoja mtu mmoja, wapo watu wamechukua fomu na wanavyeo vingine waacheni  vikao vyetu ndio umadhubuti wa chama chetu tutawafundisha katiba ya chama chetu inasema nini."

Ndugu Polepole amemaliza kwa kuwaasa wakazi wa pwani wasiwe na wasiwasi waamini kazi ya serikali yao na chama chao kwani muelekeo ni mzuri na unatia hamasa.

No comments:

Post a Comment