Ndugu watanzania wenzangu naomba kutumia nafasi hii kuwajulisha pia kukanusha uvumi na taarifa inayoenezwa katika mitandao ya kijamii kumuhusisha Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) na masuala ya Ardhi huku akidaiwa kumpinga Waziri wa Ardhi na Makaazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Kaimu katibu Mkuu Leo Julai 16, 2017 amewasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku tano.
Nawaomba muisome na kuipuuza taarifa hiyo ya uzushi, najua maneno hayo yamenezwa na maadui na mabingwa wenye uhodari wa kususia chaguzi ili kutafuta umaarufu wa kisiasa na kuwafariji wafuasi wao.
Kaimu Katibu Mkuu wetu hana nidhamu ya kipumbavu wala uthubutu wa kijinga kutamka lolote ambalo liko nje ya mamlaka yake na hasa katika mambo yanayohusu Serikali zetu na taaswira nzima ya Muungano wetu kama ambavyo malofa hao wanaovyojitahidi kutaka kumpaka matope na kumzushia uongo kama ilivyo kawaida yao.
Kimsingi hatarajii, hafikirii na hana mawazo ya kuzumgumzia suala lolote la kiserikali kwa njia ambayo si sahihi hasa ya kupinga au kukanusha masuala ya kiserikali kwa njia kama hiyo inayotaka kutumiwa na makuhani wa uongo ili kuwagonganisha viongozi wa serikali na jumuiya yetu.
Taarifa hiyo inayoenezwa ni ya kupikwa na maadui, haina mashiko wala mizania, isomeni kisha itupeni kapuni kwasababu imeandikwa na malofa wa mawazo na fikra ambao hawana kazi zaidi ya kuwayumbisha na kuwapotezea muda watanzania.
Kaimu Katibu Mkuu wetu anaendelea na shughuli zake za kikazi Mkoani Kigoma ambapo atakutana na kuzungumza na wanachama wa CCM na jumuiya zake, makundi ya vijana, kutembelea miradi ya maendeleo, kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 hivyo hahusiki na taarifa hiyo.
Mabingwa wa kuzua ambao hawana kazi ya kufanya, waendelee na kazi yao ya uzushi, kupanga utapitapi na kueneza katika jamii huku wakitakiwa kufahamu kuwa viongozi wa serikali, chama na jumuiya zake wako makini na katu hawatafarakana au kuvutana mashati kama maadui wanavyofikiria.
Mwisho tunawaomba wananachi wa Tanzania Bara na Zanzibar waendelee na kazi zao za uzalishaji mali na ujenzi wa Taifa letu iachane kabisa na maneno hayo ambayo hayana ukweli wowote wala msingi.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Jokate U. Mwegelo
Katibu Uhamasishaji Na Chipukizi
16/07/2017.
No comments:
Post a Comment