Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameanza ziara ya Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini sambamba na kusikiliza Kero za Ardhi kwa wananchi wa maeneo mbalimbali akianza na mkoa wa Kigoma tangu mwezi Julai 11, kabla ya kuendelea na mkoa wa Mwanza Julai 24 , na baadae Mikoa ya Geita, Shinyanga na Simiyu
Akiwa mkoani Kigoma wilaya ya Kasulu Mhe Dkt Angeline Mabula amezungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mwandiga Waliokuwa wakikabiliwa na mgogoro wa muda mrefu wa Ardhi baina yao na mmiliki wa shule ya Goseso Kwa kutwaa eneo la wananchi hao bila kuwalipa fidia na kuliendeleza kwa muda mrefu ambapo Naibu Waziri huyo wa Ardhi akaamlisha kurejeshwa mara moja kwa eneo hilo kwa wananchi au kulipwa fidia
‘… Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Magufuli imedhamiria kumaliza kabisa migogoro ya Ardhi na changamoto zake, Hivyo niombe tu hii migogoro isiyo na tija haiwezi kukubalika kama umepewa eneo ni lazima kwanza uliendeleze lakini pia ulipe fidia kwa wenye eneo uliowakuta tofauti na hapo ni bora ukalirejesha …’
Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula amewasisitiza wananchi hao juu ya umuhimu wa zoezi la urasimishaji wa makazi sambamba na umilikishwaji wake kisheria huku akiwaasa kuacha kuwa na matumizi mabaya ya Ardhi yasiyozingatia taratibu na sheria
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Mwandiga Mbali na kumshukuru Naibu Waziri wa Ardhi Mhe Dkt Angeline Mabula na Serikali ya awamu ya Tano kwa ujumla wake kwa utendaji wake wa kazi hasa kumaliza mgogoro huo wa muda mrefu uliokuwa ukiwasumbua wameahidi kuwa watazingatia sheria na taratibu za Ardhi huku wakifurahisha na zoezi la Urasimishaji linalolenga kuwasaidia wananchi wengi waliojenga bila kufuata utaratibu na matumizi bora ya Ardhi
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
15.07.2017
No comments:
Post a Comment