Saturday, July 22, 2017

POLEPOLE: WASIOTENDA HAKI KUKATWA KWENYE CHAGUZI ZA CHAMA NGAZI ZOTE

Ndugu Polepole Katibu wa halmashauri Kuu, itikadi na uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM) alifanya ziara ya kichama wilaya ya Ilala alipata fursa ya kuzungumza, kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za uchaguzi zinazoendelea pamoja na changamoto zinazohusu usimamizi wa miradi na mali za chama.

Ndugu Humphrey Polepole amekutana na halmashauri kuu za matawi na wajumbe wa kamati ya siasa za matawi na kata za gerezani na ilala pia ziara hiyo ilihudhuriwa na  katibu wa  CCM wilaya ya ilala Ndugu Joyce Mkaugala pamoja na mbunge wa jimbo la ilala Ndugu Mussa Zungu.

Katika uimarishaji wa chama na kuhakikisha haki inatendeka katika chaguzi zinazoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi Ndugu Polepole alifanya ziara hiyo baada ya kupokea  taarifa ya muenendo wa uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi kata ya ilala na kata ya gerezani.

Katika kata ya gerezani malalamiko yalikuwa mengi ikiwemo, nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata  kurudi jina moja na kupitishwa bila kujadiliwa na kamati ya siasa ya kata, pia uongozi wa kata kutosoma mapato na matumizi ya fedha za chama katika kamati ya siasa ya kata, mambo hayo  ni kinyume na taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ndugu Polepole ameagiza kikao cha kamati ya siasa wilaya ya ilala kuwasimamisha uongozi wajumbe wa kamati ya siasa ya kata ya gerezani kwa kushindwa kutoa uongozi,kuendesha kata na kusimamia na kuendesha mali na miradi ya chama kata ya gerezani.

Pia Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kata ya ilala  na mwenyekiti wa jumuia ya wa wanawake (UWT) kata ya ilala  wamejiuzulu nafasi zao kwa hiari kutokana  na kukiri udhaifu ulipo kata ya ilala katika  eneo la  uongozi, usimamizi wa mali za chama, migogoro  ya wanachama na viongozi, kutetereka kwa haki kwenye chaguzi za matawi na mashina pamoja na mambo mengine mengi.

“Uimara wetu CCM unatatokana na ubora wa viongozi wetu tutakaowachagua” alisema ndugu polepole kwa kumalizia.

Ziara hizi za viongozi wa kitaifa wa Chama Cha Mapinduzi kutembelea wanachama na viongozi wa ngazi za msingi ni muendelezo wa viongozi hao kusisitiza na kusimamia agenda ya mageuzi makubwa yanayofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

No comments:

Post a Comment