Saturday, July 22, 2017

ZENDA AFANYA KIKAO NA WANAVYUO WA VYUO NA VYUO VIKUU UKUMBI WA MIKUTANO UVCCM UPANGA

Zifuatazo ni nikuu za Kaimu Katibu wa Idara ya vyuo na vyuo vikuu UVCCM Taifa Komrade Daniel Zenda akiwa katika kikao na wana vyuo wa vyuo vikuu Mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano UVCCM Upanga.

1. "Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 36 inampa Rais mamlaka ya kuanzisha na kuwateua watu wa kushika nafasi za madaraka"- Daniel Zenda

2." ukisoma ibara ya 36 kifungu kidogo cha pili kinasema Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika nafasi za madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera za idara za taasisi za Serikali na watendaji wakuu wanaowajibika kusimamia utekelezaji wa sera za idara hizo " - Daniel Zenda.

3." Sisi kama vijana wasomi tunapenda kuwaambia watanzania Tundu Lisu ana maneno ya uchochezi yenye lengo la kuligawa Taifa kwa hiyo tumpuuze "- Daniel Zenda.

4."Tunawaomba wana Singida Mashariki wasifanye tena makosa kutuletea viongozi wanaoleta ukabila na ukanda kama Tundu Lisu"  -  Daniel Zenda.

5. " IGP (mkuu wa polisi)  anawajibika chini ya Wizara ya Mambo ya ndani inayoongozwa na Waziri Mhe. Mwigulu Nchemba anayetoka Singida na Naibu Waziri anatoka Dodoma hapo ukanda upo wapi?"  Daniel Zenda.

6. " CDF (Mkuu wa majeshi) aliwajibika chini ya Wizara ya ulinzi inayoongozwa na Waziri Dkt. Hussein Mwinyi kutoka Zanzibar hapo ukanda upo wapi?" -  Daniel Zenda.

7. "Tukiangalia uteuzi wa Mawaziri, wakuu wa Wilaya, wakurugenzi na makatibu tawala wote wametoka sehemu mbalimbali za nchi "- Daniel Zenda.

8. "Watanzania wafahamu kuwa Rais katika teuzi zake anazingatia uwezo wa mtu bila kujali, Chama, dini wala kabila " - Daniel Zenda.

9." Siasa ni kama dawa ikifika wakati zinaisha muda (expire), kuna dalili zote za kuexpire kwa wanasiasa wa aina hiyo " - Daniel Zenda.

10. "Pia napenda kusema kuwa wana vyuo tunampongeza Rais kwa kuwapa dhamana ya uongozi vijana ambao mpaka sasa hawajatuangusha" -  Daniel Zenda.

11. "Vijana wasomi wa vyuo na vyuo vikuu tuna imani kubwa na Rais wetu kwa yote anayoyafanya" -  Daniel Zenda.

No comments:

Post a Comment