Kesi
inayomkabili Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF, Jamali
Malinzi na wenzake imeendelea leo July 31, 2017 katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu na kusogezwa tena mbele hadi August 11, 2017 kwa
sababu upelelezi haujakamilika.
Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga amedai mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na
kwamba upelelezi haujakamilika ambapo hata hivyo, Mawakili wa
washtakiwa, James Bwana na Abraham Senguji hawakuwa na pingamizi na
suala la upelelezi.
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi August 11, 2017.
No comments:
Post a Comment