Tunaendelea kuchukua hatua ili kuhakikisha watanzania wanapata huduma za matibabu bila vikwazo!
Leo nimezindua *TotoAfyaKadi!* Bima ya Afya kwa watoto. Kwa mujibu wa Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), kati ya Watanzania 52m waliopo sasa (2017) *watoto ni 26.7m (sawa na 51%)*. Mtoto ni mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18.
#TotoAfyaKadi ni njia sahihi ya kuelekea Bima ya Afya kwa Wote nchini. Mpango huu unatoa Uhakika wa Matibabu kwa mtoto kwa *Tshs 50,400/=* kugharamia matibabu yake kwa mwaka mzima. Tena sio kwa Vituo vya Serikali bali pia vya Binafsi. Lakini pia si kwa Halmashauri au Mkoa unayoishi bali nchi nzima.
Wazazi/Walezi wenzangu; *Ugonjwa huja bila Taarifa!* Tuchangamkie #TotoAfyaKadi ili kuwa na uhakika wa matibabu ya Mtoto kabla ya kuugua. Mwenye Macho haambiwi Tazama. #TotoAfyaKadi ndio mpango mzima.
Ummy Mwalimu,Mb
WAMJW
31 July 2017
No comments:
Post a Comment