Na Margareth Chambiri, NEC
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekishauri Chama cha Wananchi (CUF)
kumaliza mgogoro unaoendelea ndani ya Chama hicho kwani unaweza
kusababisha kupoteza nafasi za Udiwani katika Uchaguzi Mdogo
unaotarajiwa kufanyika wakato wowote kuanzia sasa.
Tahadhari
hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Kailima
Ramadhani katika mahojiano maalum Ofisini kwake kuhusu tuhuma
mbalimbali zilizoelekezwa Tume hiyo ikiwemo suala la Uteuzi wa Wabunge
wa Viti Maalum kupitia CUF.
Bw.
Kailima amesema mvutano unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF)
hauna tija, hivyo ameshauri pande mbili zinazovutana kukutana na
kumaliza tofauti zao kwani hali hiyo itawanyima nafasi ya kutoa wagombea
kwenye uchaguzi huo mdogo.
“Mimi
niwashauri, CUF wana mgogoro wao wamalize mgogoro wao. Ni vizuri
wakutane wamalize mgogoro wao kwani hii inaweza kuwaletea matatizo
wagombea wakati wa Uchaguzi.’ alisesema Kailima na kusisitiza kuwa mgogoro ndani ya chama hicho hauna tija na badala yake unakidhoofisha.
Amesema
Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, inakitaka Chama cha Siasa kumsimamisha
Mgombea mmoja kwa nafasi moja, lakini pia mgombea wa nafasi ya Rais na
Mbunge lazima fomu yake isainiwe na Viongozi wa ngazi ya Taifa
wanaotambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.
"Lakini
ukisoma Maelekezo ya Vyama vya Siasa na Wagombea yanasema iwapo chama
cha Siasa kina mgogoro ni lazima fomu zake zisainiwa na kiongozi wa juu
wa ngazi ya Mkoa, sasa kwa hali hii iwapo CUF wasipokutana watapoteza
nafasi." Amesema Mkurugenzi huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Bwana
Kailima amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatambua taarifa za Vyama
vya Siasa iliyowasilishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa na kwa Chama cha
CUF viongozi wanaotambuliwa na Tume hadi hivi sasa ni Mwenyekiti Prof.
Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu ni Maalim Seif Sharif Hamad.
"Tume
inatambua kuwa Mwenyekiti wa CUF ni Prof. Ibrahim Lipumba, Inatambua
Katibu Mkuu wa CUF ni Maalim Seif Sharif Hamad na Naibu Katibu Mkuu
upande wa Bara ni Magdalena Sakaya" amesema.
Amesema
Tume haijazuiliwa na Mahakama wala na Msajili wa Vyama vya Siasa kwamba
isifanye mawasiliano na Viongozi hawa, na kubainisha kuwa Tume
itaendelea kufanya mawasiliano na Viongozi mpaka hapo itakavyoelekezwa
vinginevyo na Msajili wa Vyama au Mahakama.
Mkurugenzi
huyo wa Uchaguzi amesema Tume inafanya kazi kwa mujibu wa Sheria,
Kanuni na Taratibu na kwamba mawasiliano ya Tume na Chama cha Siasa ni
kwa mujibu wa maelekezo ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye ndiye
anayesajili Vyama vya Siasa nchini.
Aidha
katika hatua nyingine Bwana Kailima ameelezwa kusikitishwa na taarifa
za upotoshaji zinazoihusisha Tume kwenye kikao cha Wanasheria kwa lengo
la kumshauri Spika wa Bunge kuhusu Chama cha Wananchi CUF na kubainisha
kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.
Akielezea
hatua zinazoweza kuchukuliwa na Tume dhidi ya upotoshwaji unaofanywa na
baadhi ya Wanasiasa na Vyombo vya Habari kuhusu utendaji kazi wa Tume
Kailima amesema Tume itatumia Mamlaka zinazohusika na usajili ingawa
hata hivyo amesisitiza kuwa ni vyema Vyama vya Siasa vitumie Wanasheria
wao kusoma Sheria na taratibu za Uchaguzi ili kupata habari sahihi.
"Hatua
ya kwanza tunayochukua ni hii ya kuelimisha Chama pengine ni bahati
mbaya lakini hatua ya pili ni ya kuzitaarifu mamlaka Kwa upande wa Vyama
ni Msajili wa Vyama kwa upande wa Vyombo vya Habari vya Magazeti
tunamtaarifu Msajili wa Magazeti ili ashughulike nao’ lakini kubwa
tunawashauri jamani someni au ulizeni Tume," amesema Kailima.
No comments:
Post a Comment