Tuesday, July 18, 2017

BUNGE LA JAMII LAJADILI KWA KINA KUHUSU KUZIMWA KWA MITAMBO YA IPTL

Na: Deus Lugaila

Bunge la jamii kupitia wanachama wake wamejitokeza wazi kujadili kuzimwa kwa mitambo ya IPTL kampuni ya kufua umeme ya INDEPENDENT POWER TANZANIA Kama Kutakuwa na madhara au la

Hali hii inajitokeza wakati mmiliki wa kampuni ya PAN AFRIKA POWER (PAP) Harbinger Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering akiwa ndani.Hatua hiyo imekuwa baada ya maombi ya kuongezeka muda wa miezi 55 ya leseni yake kusubiria uamuzi wa ikulu.

Akiongoza kikao cha Bunge la jamii,Katibu kiongozi wa Taasisi hiyo ya kijamii Rajabu Jumanne amewapa Uhuru wanachama kujadili kwa kina swala hilo huku wanachama wengi Wakidai kuwa kama serikali imeona vema kufanya hivyo basi ifanye ili kuweka mambo sawa, "Ni bora kupata hasara ya muda mfupi na kuokoa pesa nyingi zilizotaka kupotea kwa ajili ya kutatua changamoto za watanzania," waliongea wanachama hao wa Bunge la jamii Katika mdahalo wao.

Lakini pamoja na hayo Bunge la jamii limejiridhisha wazi na kuwa uamzi wowote wa serikali ni mzuri kwani serikal kufanya kitu Fulani tayar imeshakifanyia uchunguzi na tathimini kutokana na wataalam waliopo,

Pia wanachama wa Bunge la jamii,wanaishauri serikali kuchukua maamuzi magumu juu ya wahujumu uchumi wa taifa bila kuoneana aibu ,maana malengo ya serikali sasa ni kuipeleka Tanzania ya viwanda na yenye uchumi wa kati.

Bunge la jamii hufanya vikao vyake kila siku kuanzia jumatatu hadi ijumaa kwa mstakabali wa taifa na watanzania.

Tanzania ya viawanda inawezekana

No comments:

Post a Comment