Friday, July 21, 2017

CCM WILAYA SINGIDA VIJIJINI YAFANYA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA WILAYA

Katika kikao hicho katibu wa CCM wilaya Bi GRACE SHINDIKA alitoa maangalizo katika uchaguzi kwa kuwataka wanachama kuwa makini na utoaji au upokeaji wa Rushwa katika  kuchagua viongozi watakaoendana na kasi ya HAPA KAZI TU.

Pia aliendelea kuwaeleza wagombea na wanachama kwa ujumla kujinasua katika Makundi ambayo mwisho wa siku yatapelekea mgawanyiko ndani ya chama.

Shindika alisema kuwa hakuna Mgombea kongozi anaeruhusiwa kuanza kampeni kabla ya muda pamoja na hilo pia alisema kuwa hairuhusiwi kufanya ziara kwa viongozi  waliochukua fomu kwani baadhi yao hutumia njia hiyo kufanya kampeni.

Aidha, Aliwasihi wasimamizi wa uchaguzi wa kata mara tu majina yatakaporudi, waanze uchaguzi mapema kabla ya saa tano asubuhi ili kumaliza mapema uchaguzi lakini pia mshindi lazima awe amepata nusu ya idadi kura.

No comments:

Post a Comment