Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, imelalamikiwa kwa kuendelea kukusanya ushuru wa mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji ambao umezuiliwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Hayo yalibaishwa hii leo na baadhi ya wakazi na wajasiriamali katika Kata ya Kakukulu wilayani humo, wakati wa ziara ya kikazi ya Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka.
Mkazi wa Kata hiyo, Kamalamo Lucas alisema anashangaa kuona gizo la Rais Magufuli ambalo amekuwa akilisisitiza mara kwa mara la kutowatoza ushuru wa mazao yasiyozidi tani moja likikiukwa huku Selman Masatu Nyamaka akieleza kusakwa na polisi kwa tuhuma za kushinikiza wanachi wasikubali kulipa ushuru wa mazao.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Ukerewe, George Nyamaha alieleza kusikitishwa na taarifa hizo na kusema kwamba baraza la halmashauri halijaidhinisha kukusanywa kwa ushuru huo na kwamba hayo yanafanywa na baadhi ya watumishi wasio waadilifu.
“Hakuna hata siku moja baraza letu limebariki kutoza ushuru, na kama jambo hili linafanyika basi ni udhaifu wa baadhi ya watendaji wanaolalamikiwa na kwa sababu nimepata taarifa hii leo, kuanzia kesho jumatatu nitaanza kufuatilia kwa ukaribu jambo hili”. Alisema Nyamaha huku akibainisha kwamba halmashauri hiyo imejaa watumishi wa muda mrefu ambao wanalalamikiwa hivyo ni vyema serikali ikawachukulia hatua kwani wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, aliwatahadharisha watendaji katika halmashauri hiyo ambao wamekuwa kikwazo katika utendaji wao wa kazi ikiwemo kuichonganisha serikali na wananchi na kutaka suala hilo kufuatiliwa kwa ukaribu ili kuhakikisha wananchi hawatozwi ushuru huo kama ilivyoagizwa na Rais Magufuli.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, akipandisha bendera baada ya kuzindua tawi la Kitanga wilayani Ukerewe. Shaka amewapokea zaidi ya vijana wapya 50 waliojiunga na CCM
Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, akizungumza wakazi wa ziara hiyo
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, akisalimiana na akina mama wajasiriamali katika soko la Kakukulu wilayani Ukerewe, amewahimiza kufanya kazi kwa bidii wakati ambao serikali imeboresha mazingira kwa wajasiriamali kufanya shughuli zao ikiwemo kuondolewa kwa tozo na ushuru kwenye mazao zao
Kikundi cha waimbaji katika Kata ya Kakukuru wilayani Ukerewe, kikiimba wakati wa kumpokea Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM, Shaka Hamdu Shaka.
Kulia ni Katibu wa UVCCM wilayani Ukerewe Ibrahim Kandumila, akitoa salamu zake. Kushoto ni Kaimu Katibu wa UWT wilayani Magu, Chuki Alex
Mwenyekiti wa UVCCM wilayani Ukerewe, Petro Misana Majula, akitoa salamu zake
Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Mwanza, Ruben Sixtus akizungumza wakati wa ziara hiyo
Baadhi ya wanachama, mabalozi na viongozi wa jumuiya mbalimbali za CCM wilayani Ukerewe
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza kwenye ziara yake wilayani Ukerewe
Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza, Mariam Amiry, akitoa salamu zake wakati wa ziara ya Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa wilayani Ukerewe
Zilipigwa ngoma za asili, ikiwa ni sehemu ya mapokezi ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM wilayani Ukerewe
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, na viongozi wengine kwa pamoja wakicheza ngoma ya dogoli
Mwenyekiti wa halmashauri ya Ukerewe, George Nyamaha, akizungumza wakati wa ziara ya Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa wilayani Ukerewe
Mwenyekiti wa CCM wilayani Ukerewe, Ally Mambile, akitoa salamu zake wakati wa ziara ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa wilayani Magu
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na wanachama, mabalozi pamoja na viongozi wa jumuiya mbalimbali za CCM wilayani Ukerewe. Shaka amehitimisha ziara yake wilayani Ukerewe na tayari amepokelewa wilayani Ilemela kwa ajili ya ziara yake kesho. Huu ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Mwanza itakayodumu kwa muda wa siku saba tangu jana Julai 22,2017 ilipoanza wilayani Magu
Credit:BMG
No comments:
Post a Comment