Friday, July 21, 2017

SHAKA AMALIZA ZIARA YA SIKU SITA MKOANI KIGOMA

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka  Hamdu Shaka (MNEC) leo amekamilisha ziara ya siku 6 mkoani Kigoma kwa kutembelea wilaya zote 7 za mkoa huo.

Katika ziara hiyo pamoja na mambo mengi alikagua na kushiriki kufanya kazi za kijamii ikiwa  ni  utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020, alishiriki kuona shuhuli mbali mbali za ushalishaji Mali kupitia makundi ya vijana na kuwasaidia kwa kuwaunga mkono ili kuongeza  mtaji  wa miradi yao, alipata nafasi ya kuzungumza na makundi ya vijana kwa nyakati tofauti,  viongozi wa CCM, jumuiya za CCM pamoja na kupokea wanachama wapya 786  kutoka vyama vya NCCR Mageuzi, CHADEMA, ACT walendo, UDP na CUF ambao asilimia 85% ni  Vijana kati yao.

Pamoja na shuhuli nyengine mbali mbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa alizoshiriki  pia alihudhuria sherehe za uwekaji wa Jiwe  la Msingi Barabara ya Nyakanazi -Kakonko - Kibondo uliofanywa na Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli katika viwanja vya kituo cha mabasi  Kankonko.

Wakati huo huo Kaimu Katibu Mkuu UVCCM kesho anatarajiwa kuanza  ziara ya siku 7 Mkoani Mwanza kwa kutembelea wilaya zote za Mkoa huo.

No comments:

Post a Comment