Tuesday, January 17, 2017

JUMUIYA YA MASINGASINGA WATOA MSAADA SEKONDARI YA KIWANGWA

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wa tatu kutoka kushoto,akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Singh Bwana Kugis wa pili kutoka kulia,pamoja Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo wa kwanza kushoto baada ya kupokea msaada wa madawati kutoka Jumuiya hiyo.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze akipanda mti kuashiria sherehe  ya miaka 350 toka kuzaliwa kwa Guru Sing Sikh.
Mh.Mbunge akipokea Madawati toka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Singh.Aliyesimama katikati ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiwangwa Ndg. Rashid
Jumuiya ya Singh maarufu kama masingasinga hapa nchini imetoa msaada wa madawati  100 na meza 100 ,vyenye gharama ya mil. 5,kwa shule ya sekondari ya kata ya Kiwangwa,chalinze wilaya ya Bagamoyo.
Jumuiya hiyo imetoa msaada huo ,ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu.
Akiongea  kwa niaba ya mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Kurgis,katibu wa Jumuiya hiyo ya Singh bw .Singh alisema ubora wa upatikanaji wa elimu katika shule unategemea mchango wa kila mdau hivyo wao wameamua kuanza na madawati .
Alisema lengo ni kuhakikisha watoto wanasoma kwenye mazingira mazuri na hatimae kutimiza ndoto zao.
,"Ndugu zangu sisi Singasinga tumeamua kuanza na madawati lengo letu ni kuona watoto wakisoma katika mazingira rafiki,hatimae waweze kufika mbali kielimu”alisema Kurgis .
Akizungumza katika hafla ya upokeaji wa madawati hayo mgeni rasmi, mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete,aliishukuru jumuiya ya Singasinga kwa msaada huo na kusema utasaidia watoto kuondokana na adha ya kukaa chini .
" Leo tunawashukuru kwa madawati lakini tatizo la maji na umbali wa wanapoenda kuchukua maji vijana wetu unasababisha pia kushuka kwa viwango vya ufaulu sio tu shuleni hapa lakini katika maeneo mengi ndani ya halmashauri yetu.alieleza Ridhiwani.
Ridhiwani aliwaomba wajaribu kusaidia changamoto hiyo kwa kuiweka kwenye mipango yao kazi ya maendeleo ya jamii.
Alifafanua endapo jumuiya hiyo itasaidia kuchimba visima italeta tija katika maeneo mengi jimboni hapo maana pia watoto wanateseka kutokana shule nyingi hazina huduma ya maji.
Ridhiwani alisema kijumla Jimbo hilo limeshakamilisha kutatua tatizo la upungufu wa madawati na wanashukuru kupata ya ziada.
Mbunge huyo alisema kwasasa nguvu zao zinaelekezwa katika ujenzi wa madarasa mashuleni na kukarabati yale chakavu hivyo aliwaomba wadau wa maendeleo wajitokeze kuunga mkono suala hilo.

No comments:

Post a Comment