Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, |
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deogratius
Ndejembi leo mapema, ametembelea Maghala ya Kuhifadhia Nafaka katika soko la
kimataifa Kibaigwa. DC Ndejembi amekagua Maghala hayo ili kujiridhisha na takwimu
za uhifadhi wa chakula katika wilaya ya Kongwa.
"Kibaigwa ni Soko Kuu la kimataifa la
Nafaka Nchini na kuna Maghala yakuhifadhi nafaka ambayo husambazwa nchi nzima
na nchi za jirani. Akizungumza na uwongozi wa Soko hilo kubwa, DC alisema.
"Nimekuja kujua kama kweli kuna Ujazo
wakutosha ktk Maghala yetu, Nimeona kuna Chakula cha Kutosha na hakuna haja
yakusikiliza maneno ya hao wanaotaka kutia Hofu watanzania yakuwa Eti Taifa
linanjaa na litakumbwa na Njaa kwa kiwango cha aina yoyote".
Wanachi wa Wilaya ya Kongwa, Mkoa wa Dodoma
na Tanzania kwa Ujumla Ondoeni Shaka Hakuna Njaa kwasababu chakula kipo. Na
Wanasiasa Acheni Kupotosha Wananchi na kuwatia Hofu.
Mbali na hayo alizidi kufafanua akasema Kuna
Hifadhi kubwa sana ya Nafaka na inazidi kutoka kuelekea maeneo mbali mbali
Nchi, kama kuna mwenye uhitaji wa Mazao ya nafaka Aje Kibaigwa Kongwa atanunua
Mazao Tani atakazo.
DC Ndejembi amesema "Kongwa kuna Vijiji
kama HembaHemba, Ngomai, Kibaigwa , Mkoka na Mlali Vijiji hivi vina Akiba
yakutosha ya Mazao ivo kwanini Mkuu wa Wilaya niseme kuna Njaa?
Alimalizia Mazungumzo yake ametoa wito kwa
Watanzania kuwa Makini na Wafanya Biashara ambao hucheza dili za kuuza Mazao na
wamezoea kuishi kwa kupewa Vibali vya serikali kwa kununua Mazao kwa bei nafuu
kisha kuwauzia Watanzania kwa bei ya Juu! Lakini wamekuwa wakiishi kwa
kuanzisha Matatizo ili kutumia Fulsa hiyo kujinufaisha wao.
DC Kasema Watanzania wawe makini sana pia na
Wanasiasa ambao wameshaanza kupita nakuwadanganya kuwa Taifa halina Chakula na
wao watawaletea Chakula huo ni uwongo mtupu.
Naomba mfahamu kuwa Mh Rais na sisi wasaidizi
wake Bado hatujashindwa kulihudumia Taifa hili.
Aliyasema Ndejembi Mkuu wa Wilaya ya Kongwa
alipokuwa Kibaigwa katika Maghala yakuhifadhia Vyakula.
No comments:
Post a Comment