Tuesday, January 17, 2017

POLEPOLE: KUTANGAZA TAARIFA ZINAZOSABABISHA TAHARUKI KATIKA NCHI NI KOSA LA JINAI



*AWASIHI WANASIASA KUJIKITA KATIKA SIASA SAFI NA UONGOZI BORA

*WASITUMIE UONGO NA SHIDA ZA WATU KUSAKA UMAARUFU WA KISIASA

Na Bashir Nkoromo
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewasihi viongozi wa vyama vya wapinzani kujikita katika siasa safi na uongozi bora, kwa kuachana na matamko ya uongo yanayosababisha taharuki katika nchi na kuchonganisha wananchi na serikali yao, kwa kuwa vitendo hivyo havina manufaa kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Huphrey Polepole, wakati akizungumza na waandishi wa habari, leo Januari 17, 2017, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, kutoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Kichama.

Polepole amsema, wapinzania wamekuwa wakitumia matatizo ya wananchi na kutoa matamko ya uongo ili kutia nchi katika taharuki kwa lengo la kujitafufia umaarufu wa siasa vitendo ambavyo alisema, havisaidii wananchi wala wanasiasa  wa vyama hivyo katika kuleta maendeleo ya nchi.

Alisema, mbali na matamko ya viongozi wa vyama hivyo kutosaidia, katika ujenzi wa maendeleo yamaendeleo ya nchijambo ambalo alisema za kueneza maneno ya yasiyofanyiwa utafiti kwa lengo la kusababisha taharuki kwa wananchi, jambo ambalo alisema, si miongoni mwa siasa safi wala uongozi bora.

Polepole alisema, wapinzani wamekuwa wakifanya siasa za aina hiyo wakiwa wanajua ubaya wake, kwa kuwa wao lengo lao ni kujaribu kuchonganisha wananchi na serikali hata pale ambapo serikali inaonyesha juhudi za dhali za kuijenga Nchi yenye uchumi imara wa viwanda.

"Nawaonba Watanzania tuwapuuze wanasiasa wa vyama hivi,  tuendelee kuiunga mkono serikali, ili itimize mipango na malengo iliyoweka, ikiwemo kuhakikisha Tanzania inakuwa kiuchumi kwa kuwa nchi ya viwanda, hali ambayo itasaidia sana kutukwamua Watanzania kutoka katika umasikini", alisema Polepole.

Polepole alitaja kuwa miongozi mwa mambo ambayo katika kipindi hiki wanayatumia kupotosha ili kujaribu kuletea taharuki wananchi ni pamoja na kueneza propaganda kuwa Tanzania imekumbwa na baa la njaa na pia kutumia matatizo waliyopata wananchi wakati wa janga la tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera kama mtaji wao kisiasa.

"Kwanza mjue, kutungaza taarifa ambazo zitaleta taharuki katika jamii ni kosa la jinai, lakini pia inajulikana na wenyewe wanajua, kwamba Duniani kote zipo taratibu ya utangazaji wa majanga katika nchi yoyote. Baa la njaa ni janga kubwa linapofikia kiwango kibaya, mwenye mamlaka ya kutangaza ni Mkuu wa nchi", alisema Polepole na kuongeza;

Alisema, Tanzania haijawahi kupata  njaa yenye kiwango cha kuitwa baa la njaa, katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, hivyo wanaojaribu kutangaza kuwa Nchi ipo katika baa la njaa ni kushindwa kufanya siasa safi na kukosa uongozi bora kama ilivyo CCM ambayo mambo hayo inayo.

"Ingawa tumekuwa na tatizo la njaa katika sehemu chache za na kuwepo upungufu wa mvua katika maeneo kadhaa ya nchi hali ambayo inaweza kusababisha upungufu wa chakula katika maeneo husika, bado hili siyo baa la njaa. Na kwa kuwa hili serikali inalijua inaendelea kuweka mazingira mazuri ili kuweza kupelekwa vyakula maeneo yote kuondoa uhaba, na kipindi hiki hatujafikia huko", alisema Polepole.

"Baada ya kuona hali ipo hivi nilitarajia viongozi wote bila kujali vyama , tuhimize wananchi kutumia chakula vizuri wasikitumie katika mambo ya anasa au kukiuza hovyo, lakini wao wanakimbilia kutangaza baa la njaa wakati njaa yenyewe haijatokea, hawa watu wa ajabu sana', alisema Polepole.

Alisema, kila kiongozi anayeongozwa na misingi ya uongozi bora na mzalendo kwa nchi yake, analo jukumu la kuwahamasisha wananchi kutunza vyakula walivyonavyo.

Kuhusu tetemeko lilitokea Bukoba  na kusababisha uharibifu na vyumba za watu na miundombinu mbalimbali alisema kama ilivyo ulimwenguni kote, inapotokea mambo haya ya majanga serikali hujenga uwezo wake kwanza ili kusaidia wananchi wake.

"Baada ya tetemeko lile, Serikali ilichofanya ni kujengea uwezo wa wananchi wasiwe mbali na huduma  ndiyo maana ikaimarisha miundombinu ya elimu, afya na barabara, kwa sababu watu waendelee kupata huduma". alimalizia Polepole

No comments:

Post a Comment