Mbunge wa jimbo la Chalinze Mkoani Pwani Mhe Ridhiwani Kikwete
MBUNGE
wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amepongeza
jitihada kubwa zinazofanywa na wataaluma wa
Halmashauri ya Chalinze katika kuboresha mradi wa
maji wa Wami kwa ajili ya wananchi wa Chalinze .
Akizungumza
baada ya kutembelea mradi huo jana Mhe Kikwete
alisema kuwa mradi huo ambao ulianzishwa na
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dkt
Jakaya Kikwete ambae ni rais mstaafu wa awamu ya
nne ni mmoja kati ya miradi bora iliyoleta ukombozi mkubwa
wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi
wa mji wa Chalinze .
Hivyo
alisema kusudi la kufanya ziara katika eneo la mradi
huo mto Wami ni kuona shughuli mbali mbali
zinazofanywa na wataalam kwa ajili ya kuendelea kuboresha
mradi huo ili kuwawezesha wananchi wake kupata huduma
ya uhakika ya maji safi na salama wakati wote.
"
Mradi huu ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa jimbo la
Chalinze na niwapongeze sana wataalam wa Halmaszhauri
kwa kazi nzuri wanayoifanya ya uboreshaji wa
maradi huu" alisema mbunge Kikwete
Alisema
kuwa amefurahishwa na jitihada zinazoendelea kufanywa
na wataalam wa Halmashauri hiyo kuhakikisha
wananchi wanapata maji na kazi kubwa yake mbunge akiwa
ni mwakilishi wa wananchi ni kuendelea kuisimamia
serikali kwa kuwawakilisha wananchi wake vema bungeni.
No comments:
Post a Comment