Saturday, December 24, 2016

HERI YA KUZALIWA KWA ASASI YA WAZALENDO NA MAENDELEO TANZANIA"AWAMATA



(Kulia) ni Chief Mrindoko Babu Mwidadi Mwenyekiti Taifa-Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) alipozuru ofisini kwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Bondeni Mhe Mbonyo

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Muhammad Shaban(Aluta.D), ambaye ni Katibu Msaidizi-Mawasiliano ya Mwenyekiti Taifa, Makao Makuu imeeleza kuwa ASASI YA WAZALENDO NA MAENDELEO TANZANIA (AWAMATA) Ilipata usajili wa kudumu mnamo tarehe 22/12/2015 na tukapatiwa usajili ooNGO/08343 Na sasa KAZI zote zitafanyika kwenye office ya Mwenyekiti Taifa na hapo ndipo kutakuwa na Makao Makuu ya AWAMAT, Ofisi hivyo ipo Mtaa wa Mbuyuni Kata Bondeni Tembo Road /Manyema Street.

Katika kipindi hiki pamoja na kuwa Asasi imeanza tu na hasa tukizingatia Asasi haina wafadhili lakini iliweza kufanya machache hasa kwa kushirikiana na kundi la Watoto ni Amana (Friends of Fatema)

 Kukabidhi tanki la maji kwa watoto kule Mtwara
Kukabidhi tank ya maji na nguo Kibaha
Kukabidhi matunda, na mswaki,chanuo,kopo la kuhifadhia chakula na mengineyo kwa watoto wenye saratani pale Muhimbili
  Kukabidhi kofia, tochi, taulo, sahani, kopo la kuhifadhia chakula, kompass box, begi na mengineyo katika kituo cha yatima cha Lady Fatema kule Kigamboni kwa awamu tofauti
Kukabidhi tank ya maji, nguo, kofia maalulum, kufanya fumigation, vyombo vya jikoni na mengineyo katika kambi ya kulea watoto wenye ulemavu wa ngozi cha Buhangija huko Shinyanga
Kituo cha watoto wenye Utindio wa Ubongo Rombo-Tank la maji lenye lita 500.
30/11/2016 AWAMATA Ilishirikia kuchangia Mchanga Roli moja la mchanga 150,000 na Roli moja Kokoto 250,000 Kwenye Mtaa wa Viwanda, Kata ya Njoro ilishiriki kwenye Serikali ya Mtaa Viwanda.

Asasi ya Wazalendo na Maendeleo na Tanzania"AWAMATA" inawashukuru wote waliofanikisha tuliyofanya kwa pamoja hasa kundi la Watoto ni Amana (Friends of Fatema) na wazalendo wote na tunatumaini ya ushirikiano zaidi hapo mbeleni kwenye kazi za kizalendo kwa namna mbalimbali.

Kwasasa Asasi inahamasisha watu kuweka oda na kulipia Tshirt za Asasi ambazo zitakuwa sare zetu wakati wa shughuli za kizalendo

No comments:

Post a Comment