Na Nathaniel Limu, Singida.
Serikali mkoani Singida, inatarajia kujenga kiwanja kikubwa cha ndege kitakachowezesha ndege kubwa za abiria na mizigo kutua, ikiwa ni maandalizi ya kunufaika na fursa lukuki za kiuchumi na kijamii zitakazopatikana,baada ya makao makuu ya nchi kuhamia jirani Dodoma.
Serikali mkoani Singida, inatarajia kujenga kiwanja kikubwa cha ndege kitakachowezesha ndege kubwa za abiria na mizigo kutua, ikiwa ni maandalizi ya kunufaika na fursa lukuki za kiuchumi na kijamii zitakazopatikana,baada ya makao makuu ya nchi kuhamia jirani Dodoma.
Hayo
yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Rehema Nchimbi wakati
akizungumza kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema
wakati wo wote kuanzia sasa kazi ya kutafuta eneo la kujenga kiwanja
hicho na taratibu zingine muhimu, zitaanza,na amewataka wananchi wawe
tayari kutoa ushirikiano.
“Msukumo
wa ujenzi wa kiwanja kikubwa cha ndege,umekuja baada ya rais
Dk.Magufuli kuutaka uongozi wa mkoa kuangalia uwezekano wa kujenga
kiwanja hicho. Ushauri au mapendekezo yanayotolewa na mkuu wananchi,
hayo ni maagizo rasmi, kwa hiyo sisi tulio chini yake, tutajitahidi
uwanja huo unajengwa haraka,” alisema na kuongeza.
“Maadamu
Rais ameona umuhimu wa uwanja huo na yeye katika serikali yake,anao
uwezo mzuri wa fedha,sisi wakazi wa mkoa wa Singida tunachopaswa
kufanya,ni kuchangamkia haraka uwanja unapatikana na ujenzi unaanza.”
Akifafanua,
alisema serikali ya awamu ya tano imelenga nchi kuwa kwenye uchumi wa
kati, hivyo kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi inayochochea
ukuaji wa uchumi, huwa haina kigugumizi katika kutoa fedha.
Akiijengea
nguvu hoja yake hiyo, mkuu huyo wa mkoa, alisema hatapenda kuona aina
yo yote ya urasimu wa kuchelewesha ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege.
Kwa
upande wa wananchi, amewataka watoe ushirikiano wa hali ya juu katika
upatikanaji wa uwanja na ushirikiano huo usiishie hapo, uendelee hadi
hapo kiwanja kitakapomalizika kujengwa.
“Mimi
nitumie fursa hii kuwasihi wananchi katika hili la ujenzi wa uwanja wa
ndege mkubwa, walipe kipaumbele cha kwanza na fidia wawe na subira.
Waamini tu kwamba ni lazima watafidiwa. Nina uhakika kiwanja
kitakapoanza kufanya kazi, wananchi watanufaika kiuchumi kwa kiwango
kikubwa, na pengine watatanza kusema kiwanja hicho kimechelewa
kujengwa,” alisema Dk. Nchimbi.
Katika
hatua nyingi, alisema Serikali yake itafanya juhudi za kuhakikisha mkoa
wa Singida, una kuwa wa viwanda vikubwa, ili kutoa nafasi makao makuu
ya nchi Dodoma, kupumua na kujikita zaidi kwenye shughuli ya kuiongoza
nchi.
“Pia
nitahakikisha mkoa wangu unakuwa na uwezo wa kujilisha na kulisha makao
makuu ya nchi. Tuna kila sababu ya kulifikia lengo hilo. Tutahimiza
kilimo cha umwagiliaji na kuchimba mabwawa makubwa kwa ajili ya kilimo
cha malisho ya mifugo,” alisema.
No comments:
Post a Comment