WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitavumilia kuona mamia ya
vijana waliofaulu mitihani ya darasa la saba na kuchaguliwa kuingia
kidato cha kwanza wanabaki nyumbani eti kwa kuwa hakuna madarasa ya
kutosha.
“Serikali
haitaridhika kuona vijana waliofaulu vizuri wanashindwa kwenda kidato
cha kwanza. Halmashauri zilijua tangu mapema ni wanafunzi wanaenda shule
za msingi kwa hiyo inataka kuona wote waliofaulu wanakwenda sekondari
kwa asilimia 100,” amesema.
Ametoa
kauli hiyo jana mchana wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa
mkoa wa Lndi mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kwenye Ikulu
ndogo wilayani Nachingwea. Waziri Mkuu amewasili wilayani Nachingwea
akiwa njiani kuelekea Ruangwa kwa mapunziko ya mwisho wa mwaka.
Alisema
Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kutoa elimu ya bure kwa kila
mtoto sasa iweje watoto wengine wanafaulu na wanashindwa kujiunga na
elimu ya sekondari.
“Tumesema
elimu ni bure hakuna sababu ya kufanya wengine wasiende shule wakati
azma ya Serikali ni kutoa elimu ya bure. Hakikisheni wote wanaingia
katika chaguo la kwanza,” alisema.
Aliwataka
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo zimefaulisha
wanafunzi lakini hazina madarasa na madawati ya kutosha warudi mezani na
kujipanga upya ili kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanapangwa na
kuanza na wenzao katika chaguo la kwanza kwani wakisubiri chaguo la pili
wanakuwa wamechelewa.
“Kama
tumepokea vijana wengi kwenye udahili wa kidato cha kwanza, ni dhahiri
kuwa ,tutapata Vijana wengi watakaomaliza kidato cha nne. Sote tunajua
kuna agizo la kila tarafa kuwa na sekondari moja ya kidato cha tano na
sita, nataka utekelezaji wa agizo hili usimamiwe kuanzia sasa.”
“Tafuteni
moja kati ya shule kwenye tarafa zenu na ipandishwe hadhi kwa kuwekewa
miundombinu inayotakiwa ya bwalo, jiko, mabweni, mifumo ya maji,
madarasa na vyoo vya kutosha,” alisema.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema atafuatilia ili abaini ni kwa nini
taasisi ya maghala ya Serikali inadai tozo kwa wakulima wanaohifadhi
mazao kwenye maghala hayo.
Waziri
Mkuu alisema atapitia sheria ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ili kuona
kama inaruhusu tozo hizo na kuangalia sheria gani inawaruhusu kutoza
kodi. Alihoji inakuwaje taasisi ya Serikali inatoza tozo kwenye maghala
ambayo yamejengwa na wananchi.
Akitoa
mfano kuhusu ghala la Liwale, Waziri Mkuu alisema: “Kuna viagency
vimeanzishwa kazi yao ni kutoza mapato tu. Inakuwaje kunakuwa na taasisi
imekaa tu na kuanza kutoza tozo kwa wananchi wanaotumia facility za
Serikali. Sheria ya kutoza tozo imetokana na nini na hizo zinakwenda kwa
nani, je srikali imeanza kufanya biashara?,” alihoji.
“Nimepata
taarifa kuwa walikuja kuzuia mazao yasitoke hadi wao walipwe, hapana
huu siyo utaratibu. Ni kwa nini tuwanyang’anye fedha wale waliojenga
ghala? Wao walijenga ghala kutokana na ubunifu halafu unasema unawapa
sh. 7/- kwa kilo wakati wewe umetoza sh.25/- kwa kilo moja. Hapana hilo
halikubaliki,” alisisitiza.
Waziri
Mkuu alisema kama Serikali inaruhusu kuwepo kwa tozo hizo kwa jambo
ambalo wananchi wamelibuni wenyewe, basi ilipaswa kudai kodi na hiyo
kodi ilitakiwa kukusanywa na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na siyo
vinginevyo.
Waziri
Mkuu alisema atafuatilia wakala mbalimbali walioanzishwa kwenye wizara
kwani kuna nyingine zinafanya kazi ambazo zilistathili kufanywa na idara
kwenye wizara mama.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
No comments:
Post a Comment