Wakati
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likisaka makubaliano mapya ya
kuendeleza usitishaji mapigano nchini Syria, Marekani imesitisha
mashirikiano yake na Urusi ikiilaumu kuendelea kuwashambulia raia.
Wakati
Earnest wa Ikulu ya White House akisema "kila mmoja ameshachoshwa na
kuivumilia Urusi", Kirby wa Mambo ya Nje amesema "huu umekuwa uamuzi
mgumu kabisa kuchukuliwa, lakini ambao umebidi."
Akisoma
tamko rasmi la serikali ya Marekani mbele ya waandishi wa habari,
Elizabeth Trudeau, amesema hakuna njia ambapo Marekani sasa inaweza
kushirikiana tena na Urusi, kwani malengo yao yanapingana.
"Kwa
bahati mbaya, Urusi imeshindwa kuheshimu ahadi zake, ikiwemo wajibu wake
chini ya sheria za kimataifa na Azimio Namba 2254 la Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa linaloidhinisha mpango wa amani wa Syria.
Pia
haikuwa tayari ama haikuweza kuhakikisha kuwa utawala wa Syria
unatekeleza mipango ambayo awali Moscow iliikubali, na badala yake Urusi
na Syria zimechagua kutumia njia za kijeshi kinyume na makubaliano ya
kusitisha mapigano," alisema Trudeau.
Hadi sasa
hakuna lolote lililosemwa kuwa ni mpango mbadala kutoka upande wa
Marekani, licha ya kuwepo uvumi kwamba huenda sasa itachukuwa hatua kali
zaidi dhidi ya Urusi, na pia washirika wake katika mataifa ya Ghuba,
yaani Saudi Arabia na Qatar, huenda wakatuma shehena za silaha kwa waasi
wanaoupinga utawala wa Bashar al-Assad nchini Syria.
Urusi yasema iko sahihi
Lakini
kwa upande wa Urusi, msimamo wake uko wazi, nao ni kuendelea kuusaidia
utawala wa Assad kuikomboa nchi nzima kutoka mikononi mwa wale inaowaita
"makundi ya kigaidi".
Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin.
Balozi wa
nchi hiy kwenye Umoja wa Mataifa, Vitaly Churkin, ambaye ndiye rais wa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu, amewaambia
waandishi wa habari kwamba hata kama Marekani inakatisha mashirikiano
yake, msimamo wa Urusi ni sahihi.
"Lau si
kujiingiza kwetu Syria, leo bendera nyeusi za IS zingelikuwa zinapepea
kote Damascus. Huo ndio ukweli wa hali ilivyo. Na huu ndio ukweli wa
mambo kwamba kundi la Nusra limeelekea mashariki mwa Aleppo. Umoja wa
Mataifa, Stefan de Mistura, amesema wazi kwenye Baraza la Usalama kwamba
nusu ya wapiganaji walioko huko ni Nusra. Wamewakamata raia mateka
huko," alisema Churkin.
Tayari
Urusi imeipinga rasimu ya azimio la kukomesha mapigano ya Aleppo
iliyowasilishwa na Ufaransa kwenye Baraza la Usalama, ikisema hakuna
kinachoweza kufikiwa kabla ya kwanza kuwamaliza magaidi walioko huko.
Na wakati
Marekani zikivutana, mpatanishi wa Umoja wa Mataifa kwenye mzozo wa
Syria, Steffan de Mistura, amerejelea msimamo wake kuwa hajavunjika moyo
na kupatikana kwa amani, ingawa hadi sasa uhalisia uko dhidi yake.DW
No comments:
Post a Comment