Wednesday, October 5, 2016

Shule ya Sekondari hii ina madarasa manne tu..!

Leo nimezuru katika Shule ya Sekondari Lighwa iliyopo Kijiji cha Mwisi Jimbo La Singida mashariki Kwa Tundu Lissu (Mb) shule hii ina vyumba vinne vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha kwanza hadi cha nne, Haina Maabara hivyo wanafunzi wanaosoma hapa hawajawahi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo tangu misingi ya dunia ilipoumbwa.

Mbunge wa Jimbo hili anaishi Dar es salaam akija Jimboni analala Guest, yeye amekuwa mbunge wa Kitaifa anafanya maendeleo ya nchi nzima ni mwanasiasa nguli anayepata umaarufu kupitia kesi anazoshinda mahakamani sio kwa kuwatumikia wananchi waliomchagua.

Walimu wa shule hii hawana nyumba za walimu, Maji wanatumia ya kwenye madimbwi, Vyoo vinakaribia kudidimia, Wananchi wanasikia kwenye taarifa za habari tu kuwa kuna maendeleo lakini wenyewe hawajafanikiwa kuyaona kwenye majimbo yao hii ni aibu kwa mbunge wa Kitaifa.

Wananchi waliambiwa na Mbunge wasichangie jambo lolote katika jimbo hilo Mdio sikatai kama wananchi wasichangie basi achangie yeye. Embu tutafakari pamoja hivi wananchi kutochangia ujenzi wa maabara ni hasara ya watoto wao au ya Mbunge wao...? Hili halihitaji hata elimu ya darasa la saba kulitambua lipo wazi kabisa.Ni elimu ya kuzaliwa tu inatumika

Binafsi naamini sasa uchaguzi ulishamalizika kinachofuata sasa ni uwajibikaji na utekelezaji wa ilani iliyopewa ridhaa na wananchi inayosimamiwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Naaaam, Ni Neno La Wakati Mwema
Mathias Canal (Sauti ya Wanyonge)
0756413465
Lighwa-Singida

No comments:

Post a Comment