Jumatatu
hii Waislamu duniani kote wanasherehekea sikukuu ya Idd El Hajj
wakiungana na wale (Mahujaji) walioko katika miji ya Makkah na Madina,
nchini Saudi Arabia wakiendesha ibada mbalimbali.
Kati ya Waislamu duniani sikukuu hii hujulikana kwa majina mbalimbali ambayo hutafsiriwa pia kwa lugha mbalimbali kama vile:
Idd-al-Adhha yaani sikukuu ya sadaka
Idd-al-Qorban sikukuu ya sadaka (kwa kutumia neno tofauti ya "sadaka" katika Qurani); Kituruki: Kurban Bayramı; Kikurdi "Cejna Kûrbanê" ;
Idd-al-Qorban sikukuu ya sadaka (kwa kutumia neno tofauti ya "sadaka" katika Qurani); Kituruki: Kurban Bayramı; Kikurdi "Cejna Kûrbanê" ;
Idd-al-Kabir au "sikukuu kubwa"; "Bari Eid" huko Uhindi na Pakistan; jina hili hutumiwa kwa sababu kati ya sikukuu mbili zinazoamriwa katika Qurani hii ni sikukuu kubwa zaidi.
Sherehe
huanza na sala ya idd katika msikiti. Mara nyingi hufuatwa na baraza au
mkutano wa Waislamu. Katika nchi nyingu huwa na kawaida kutembelea pia
makaburi ya marehemu.
Kila
Mwislamu mwenye uwezo hupaswa kumchinja mnyama wa sadaka siku hiyo mara
nyingi kondoo lakini kuna pia sadaka za mbuzi, ng'ombe au ngamia
kufuatana na uwezo na kawaida ya nchi.
Sehemu ya nyama ya sadaka hizo hugawiwa kwa maskini wasio na uwezo. Mengine hutumiwa kwa karamu ya familia
Idd
husheherekewa kati ya tarehe 10 hadi 13 ya mwezi wa Dhul Hijjah wa
kalenda ya Kiislamu. Tarehe hali halisi hutegemea na kuonekana kwa
hilali au mwezi mwandamu. Hapa hutokea tofauti za kila mwaka kati ya
Waislamu. Kimsingi mapokeo ya kiislamu hudai kuonekana kwa mwezi kwa
macho.
Kubadilika kwa tarehe katika kalenda ya jua
Katika
kalenda ya Gregori ambayo ni kalenda ya kawaida tarehe za Kiislamu
hubadilika kila mara kwa sababu mwaka wa kiislamu hufuata kalenda ya
mwezi lakini kalenda ya kawaida hufuata jua.
Kalenda ya Kiislamu ni
takriban siku 11 kasoro ya kalenda ya jua. Kila mwaka tarehe ya Idd
huweza kutokea kwa siku mbili tofauti za kalenda ya Gregori kwa sababu
kawaida ya Uislamu hufuata kuonekana kwa mwezi kunachopatikana tofauti
duniani. RFI
No comments:
Post a Comment