Waziri wa
Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akikata utepe kuzindua
mpango huo kwa ajili ya mikoa ya Iringa na Njombe katika viwanja vya
Mwembetogwa mjini Iringa
Waziri wa
Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amesema Serikali ya
Awamu ya Tano imedhamiria kuwasajili watoto wote nchini wenye umri chini
ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa.
Dhamira
hiyo ya Serikali inalengo la kuiondoa nchi katika takwimu zinazoonyesha
kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwisho barani Afrika ambazo watoto
hawana vyeti vya kuzaliwa.
Dkt
Mwakyembe amesema hayo mjini iringa alipokuwa akizindua kampeni ya
uandikishaji watoto chini ya miaka mitano katika mikoa ya Iringa na
Mbeya iliyofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa.
Dkt
Mwakyembe ameelezea kusikitishwa na kitendo hicho cha kuwa miongoni mwa
nchi ambazo watoto wake hawajasajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa na
kusema kuwa ndio maana kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikaamua
kuendesha kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano.
Amesema
serikali imedhamiria kuiondoa Tanzania katika hali hiyo kwakuwa sio
sahihi kwa nchi kuwa katika nafasi hiyo sawa na Somalia
‘Hali hii
sio sahihi, Tanzania haistahili kuwepo katika kundi hilo tumedhamiria
kuiondoa nchi huko, tunataka Tanzania iwe juu ktk usajili wa watoto kama
ilivyo juu kwa chanjo mbalimbali kwa watoto wetu’ alisema.
No comments:
Post a Comment