Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 16 kutoka kwa
Dkt. Ave Maria Semakafu (kulia), Berious Nyasebwa (wapili kushoto) na
Benjamin Thomson wote kutoka Group la Whats App la Leaders Forum ukiwa
ni mchango wa group hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani
Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar
es salaam Septemba 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwashukuru viongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya
ambao walitoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa waathirika wa tetemeko
la ardhi mkoani Kagera, Septemba 22, 2016. Makabidhiano hayo yalifanyika
ofisini kwa Waziri Mkuu jijini .Kutoka kushoto ni Sheikh Tahir Mahmood
Chaundhry, Issa Mwakitalima, Khuram Shahzad na Jamil Mwanga. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mchango wa tani 40 za saruji zenye
thamani ya shilingi milioni 16.5 kutoka kwa Dhruv Jog na Lebulu Victor
(kulia) wote wa Kampuni ya ujenzi a Advent ukiwa ni mchango kwa
waahirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera Septemba 22, 2016.
Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es
salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 100 kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VODACOM TANZANIA, Bw. Ian Ferrao
(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia ukiwa ni
mchango kwa waarhirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Ofisini kwake
jijini Dar es salaam Septemba 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa
Meneja wa Kanda wa LAPF, Amina Kassim (kulia) na Kafiti Kafiti wa LAPF
ukiwa ni mchango wa Mfuko huo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi
mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu
jijini Dar es salaam Septemba 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea sehemu ya msaada ya vyakula wenye
thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa viongozi wa Mfuko wa Kimataifa
wa Art of Living ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi
mkoani Kagera, Septemba 22, 2016. Kutoka kushoto ni Nishitha
Kulshreshtha, Nishit Patel, Neha Movaliya,Sharik Choughule ambaye pia
ni Mwenyekiti wa CCM wa Shina la Pamba Road, Upanga na Neha Movaliaya.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
TAASISI
sita zikiwemo za dini na kijamii zimechanga jumla ya sh. milioni 172.5
zikiwa ni misaada kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi
lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu.
Mchango
huo umepokelea leo jioni (Alhamisi, Septemba 22, 2016) na Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini
Dar es Salaam.
Akikabidhi
hundi kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Bw. Ian Ferrao
alisema kiasi cha sh. Milioni 100 kimekusanywa kutoka kwenye mfuko wa
Vodacom Foundation pamoja na wadau wao.
Bw.
Ferrao amesema kampuni ya Vodacom imekuwa mstari wa mbele kusaidiana na
Serikali katika uboreshaji wa miradi mbalimbali za kijamii.
Taasisi
nyingine iliyochangia ni Mfuko wa Pensheni wa LAPF ambapo Meneja wa
Kaya ya Dar es Salaam, Amina Kassim amemkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh.
milioni 20.
Pia
Jumuiya ya Kiislam Ahmadiyya imekabidhi msaada wa sh. milioni 10 kati ya
hizo sh. milioni nne ni fedha taslimu na zilizobaki ni mabati na mifuko
ya saruji.
Naye
Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Advent, Dhruv Jog amemkabidhi Waziri
Mkuu msaada wa tani 40 za saruji yenye thamani ya sh. milioni 16.5 na
kusema kwamba wameshtushwa na tukio hilo na tayari saruji hiyo imeanza
kupelekwa Kagera.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Taasisi ya kimataifa ya Art of Living, Neetu
Kulshreshtha wametoa msaada wa vyakula mbalimbali pamoja dawa vikiwa na
thamani ya sh. milioni 10.
Dk. Ave
Maria Semakafu amemkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh milioni 16 kwa niaba
ya makundi mawili ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp. Makundi hayo
yanaitwa Leaders na Uongozi.
Akitoa
shukrani kwa waliotoa michango yote hiyo, Waziri Mkuu amewashukuru kwa
misaada hiyo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo
inafikishwa Kagera kwa walengwa.
“Tunashukuru
sana kwa michango yote. Tunashukuru na makundi ya WhatsApp ya Leaders
na Uongozi ambayo nayo yameamua kuja kutuchangia. Michango hii
inaonyesha kuguswa na mapenzi ya dhati kwa waliopatwa na maafa,”
amesema.
Waziri
Mkuu amesema Serikali inakamilisha tathmini ya maafa hayo na kuahidi
kutoa taarifa ya kiasi kilichokusanywa na kiasi kilichotumika. Amewaomba
wananchi waliotoa ahadi zao za michango wakamilishe ahadi zao.
Akaunti
ya maafa imefunguliwa katika Benki ya CRDB yenye Namba. 015 222 561 7300
kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz na namba za simu
za mkononi zinazotumika kupokea michango hiyo ni 0768-196-669 (M-Pesa), au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616(Tigo Pesa).
Tetemeko
hilo lililotokea Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo
vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa kati yao watu 253 walifikishwa
Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 walitibiwa na kuruhusiwa na
wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa
upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment