Mapigano mapya Syria
Jeshi la
Syria limetangaza kuwepo kwa mapigano mapya makali, kutaka kurudisha
eneo linalodhibitiwa na waasi huko Aleppo, ambako takriban watu laki
mbili na nusu wamezingirwa.
Jeshi hilo limewataka pia raia kujiepusha kuwa katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi.
Limesema njia za kutoka katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi zimewekwa wazi kuruhusu watu kutoka.
Tangazo hilo limekuja siku chache baada ya kushambuliwa kwa eneo hilo linalodhibitiwa na waasi, mashariki mwa Allepo.
Katika
hatua nyingine Marekani na Urusi zimeshindwa kukubaliana jinsi ya
kuufufua upya mkataba wa kusitisha mapigano, nchini Syria.
Akizungumza
baada ya mkutano wao mjini New York, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa
Marekani, John Kerry amesema Urusi inatakiwa kuonesha umakini wake
katika kumaliza ghasia nchini Syria.
''Iwapo Urusi itatujia na mapendekezo yenye kujenga tutawasikiliza. Watu
wanahitaji kuamini kwa vyovyote vile inastahili kubadilisha mbinu za
upigaji mabomu uliopo sasa ambazo zinaleta maafa na zenye kutatiza, kwa
kubadili mbinu hizo tunaweza kupata ufumbuzi...''
Amesisitiza
kuwa njia pekee ya kuonesha uaminifu ni kuacha mashambulizi ya nga,
vinginevyo amesema mazungumzo mengine yatakuwa hayana msingi. BBC
No comments:
Post a Comment