NA RAYMOND MINJA IRINGA
Timu ya Lipuli FC(Wanapuliengo )yenye maskani yake mjini
Iringa imepania kuzinyakuwa pointi tatu kutoka kwa African Sports, ambao
watakutana katika mchezo wa kwanza wa Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara
,unaotarajiwa kuchezwa September 24 mwaka huu katika uwanja wa kichangani mkoni
Iringa .
Akizungumza na Bigwa katibu mkuu wa timu hiyo Wille Chikweo alisema maandalizi
yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kuipokea timu hiyo kwa heshima ilipotokea jijini Dar Eesalam ilimokuwa
imeweka kambi yake kwa muda na usajiliChikweo alisema kuwa jambo kubwa wanalojivunia na linalowaminisha kufanya vema na hatimaye kucheza ligi kuu ni kuwa na vijana chipukizi watakaokiongoza kikosi hicho na vijana hao wanacheza kwa nia moja ya kushinda kwa kuwa wameufuta mpira na sio mpira kuwafuata jambo ambalo
linawaminisha kuwabamiza African Sports katika mchezo wa kwanza
“Kwanza niwashukuru wadau wote walioshiriki katika kuisaidia lipuli mpaka hapa ilipofika ,nimshukuru Madam Jeska Rais wa lipuli, mwenyekiti Kuyava ,wadau wakubwa wa Lipuli waliotoa hata wazo la kuisaidia lipuli kwani kwa sasa tumeanzisha kampeni ya (SAIDIA LIPULI BUKU) ambapo unaweza kuichangia kwa kupitia simu ya mkonini ambayo ni 0769442945na utakuwa umeisaidialupuli moja kwa moja kwa kweli wamefanya kazi kubwa sana niwaombe wana Iringa wote kwa pamoja na wanahabiri tuisadie lipuli iweze kufanya vema na hatimaye tucheze ligi kuu ”
Kwa upande wake Raisi wa heshima wa timu hiyo Jeska Msambatavangu alisema kuwa endapo wanairinga na wadau wa soka wataunganisha nguvu kwa pamoja wanamini timu hiyo itafanya vema na hatimaye kucheza ligi kuu
Jeska alisema kuwa yeye kama mdau wa soka na Rais wa Timu kwa
kushirikiana na wadau wote atahakikisha wachezaji wa timu hiyo wakwaziki kwa
namna yoyote wakiwa kambi ili isiwe
sababu ya kutokufanya vema wawapo uwanjani
“African Sports kitu gani nyie chezeni soka linaloelewaka
hawa tutawaweka pembeni tu tenaq munabahati mumupata mlezi ambaye ni mama
unajua mama huwa na huruma kwa wanewe sasa wewe ukoina unahitaji kiatu halafu
labda hujapahatika kuniona siku mbili tatu mana niko bize kidogo wewe chora
mguu kwenye karatasi waambie hawa viongo mpelekeni mama ahh dakika moja utapata
chezeni kabumbu safi ondoeni shaka ”
Timu hiyo ya Lipuli kwa sasa imrweka kambi yake wilayani kilolo katika kijiji cha kilole ambako huko wamepata udhamini wa nyumba waliyopewa na paroko wa eneo hilo pamoja na uwanja wakisubiri kuja kukipiga na African Sports
Timu hiyo ya Lipuli kwa sasa imrweka kambi yake wilayani kilolo katika kijiji cha kilole ambako huko wamepata udhamini wa nyumba waliyopewa na paroko wa eneo hilo pamoja na uwanja wakisubiri kuja kukipiga na African Sports
No comments:
Post a Comment