Kikosi
cha mauzo na usambazaji kutoka DARBREW katika picha ya pamoja wakiwa
wameshikilia vipeperushi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Five Star
Kikosi
cha mauzo na usambazaji kutoka DARBREW katika picha ya pamoja wakiwa
wameshikilia vipeperushi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Five Star
Dereva kutoka Idara ya Usambazaji akionyesha kipeperushi cha kampeni ya 5 star.
Wengi wafurahia kupata kinywaji katika mazingira ya usafi
Kampeni
ya uhamasishaji utumiaji wa bia ya asili ya Chibuku Super inayojulikana
kama ‘Five Star’ inayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam na sehemu
mbalimbali kinapopatikana kinywaji hiki inazidi kupamba moto na
inaendelea kuwezesha wananchi wengi kuelewa ubora wake na kwa jinsi gani
kinaleta burudani sambamba na kupunguza gharama za maisha.
Jina la
Five Star au Nyota Tano kwa Kiswahili katika kampeni hii ambapo kila
nyota inaeleza hali halisia wa bia hii ya asili na ubora wake katika
kuitumia.
Nyota ya
kwanza inaelezea kuwa Bia ya asili ya Chibuku ni Bia ya asili ya
Kiafrika kutokana na jinsi inavyokubalika katika nchi mbalimbali za
Afrika kwa kutumiwa na wengi kama kiburudisho baada ya saa za kazi.
Nyota ya
pili inaelezea vionjo vyenye kiwango cha juu vya bia ya Chibuku
vinavyotokana na mchanganyiko wa malighafi za nafaka zinazotumika
kutengenezea kinywaji hiki Nyota ya
tatu inaelezea radha inayoridhisha ya bia ya Chibuku ambayo inapendeza
mdomoni na kuleta raha na burudani ya aina yake.
Nyota ya
nne inaelezea ubora wa hali ya juu wa bia ya asili ya Chibuku kutokana
na kutengenezwa kitaalamu na kuwa na viwango vinavyotakiwa vya ubora
usioleta madhara kwa mtumiaji
Nyota ya
tano inaelezea kuwa bia ya Chibuku ni kwa ajili yetu sote kutokana na
ubora wake inaweza kutumiwa na watu wenye mitindo ya maisha ya aina
mbalimbali pia inapatikana kwenye chupa zenye ujazo wa aina
mbalimbali,hali ambayo inawezesha mtumiaji kukipata kinywaji hiki
kulingana na mfuko wake ulivyo.
No comments:
Post a Comment