![]() |
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa
Salum akionyesha gazeti la Tanzania Daima kwa waandishi wa habari,liloandika taarifa sio za kweli. |
Na Sheila Simba &
Abushehe Nondo
Viongozi wa Dini
nchini, wamesema Rais JOHN MAGUFULI Hajakataa kuzungumza wala kuwapuuza
viongozi hao ambao wamemuomba kukutana naye, kama inavyoenezwa na baadhi ya
vyombo vya habari.
Akizungumza leo jijini,
Dar es Salaam na waandishi wa habari Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa
Salum, amesema taarifa zilizochapishwa na gazeti la Tanzania Daima la Septemba
21 ISSN 0856 9762 toleo na.4310 sio za kweli.
“taarifa hizo sio za
kweli, taarifa hizo zimelenga kumgombanisha Rais na Viongozi wa Dini na
watanzania kwa ujumla na hilo halitafanikiwa,” alisema Sheikh Alhad
Aidha Viongozi hao
wamesema uamuzi wao wa kumuomba Rais kuonana naye, haujatokana na kuagizwa na
UKAWA, bali umetokana na maono waliyopewa na Mwenyezi Mungu.
Amefafanua kuwa Rais
MAGUFULI anawaheshimu Viongozi wa dini na mara zote amekua akiwaomba wamuombee
na kusema leo ni siku ya tano tangu wamuandikie barua ya kumuomba kukutana naye
na wanaimani Rais atakutana na Viongozi hao.
Ameeleza kuwa Barua hiyo
imeandikwa Septemba 19 na kupelekwa siku hiyo hiyo Ikulu, ikiwa imesainiwa na
Katibu Mkuu wa Bakwata, Katibu Mkuu wa CCT na Katibu Mkuu wa TEC.
“Naomba watanzania
wasisikilize maneno hayo kwasababu hayana nia njema kwa Taifa letu, naamini Mh
Rais tutaonana nae na tutaongelea mustakbali wa nchi katika mambo mbalimbali,” alisistisa
Sheikh Alhad
Akizungumzia utendaji wa Serikali ya Rais
MAGUFULI, Sheikh ALHAD amesema Rais amerejesha nidhamu Serikalini, ukusanyaji
mapato umeimarika na pia pengo kati ya wasionacho na walionacho linaanza
kupungua.
No comments:
Post a Comment