ABIRIA wanaotumia usafiri wa treni inayofanya safari kati ya
Stesheni, Dar es Salaam na Pugu, wataanza kulipa nauli ya Sh 600 baada
ya nauli hiyo kupitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu
na Majini (Sumatra).
Awali treni hiyo ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ilikuwa ikitoza Sh
400 kwa mtu mzima na mwanafunzi Sh 200 wakati treni hiyo ilipokuwa
katika majaribio.
Wanafunzi watalipa Sh 100 kutoka kituo kimoja hadi kingine.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Ng’hwani Rashid amesema, kampuni hiyo
ilikuwa ikitoza Sh 400 wakati ikisubiri kukamilika kwa mchakato wa
ukokotoaji nauli ambao umesimamiwa na Sumatra.
No comments:
Post a Comment