Mtaturu akisikiliza kwa makini moja ya ushauri uliopatiwa na wazee baada ya kikao kumalizika
Dc Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kikao
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na wakuu wa
idara Wilayani humo wakisikiliza kwa lakini maelekezo ya kiutendaji
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu
amekutana na zaidi ya wazee 137 kutoka vijiji 101 vilivyopo katika Wilaya ya
Ikungi, Mkoani Singida.
Katika mazungumzo ya mkuu huyo wa Wilaya na wazee hao
yalijikita zaidi katika kujadili namna ya kukabiliana na umasikini kupitia
nguvu Kazi ya Taifa (Vijana) katika kilimo na ufugaji wa kisasa.
Dc Mtaturu amewasilisha dhamira ya serikali ya Hapa Kazi Tu
chini ya Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Joseph Pombe Magufulu kwa wazee wa
Wilaya ya Ikungi na Taifa kwa ujumla ni kupambana na mafisadi, Rushwa na
wahujumu uchumi ili kuboresha huduma za Jamii ikiwemo Afya hususani katika
kuboresha huduma za Afya kwa wazee wote nchini sawia na Wanawake wajawazito na
watoto.
Katika kuhakikisha kunakuwa na chachu ya maendeleo
kwaMapinduzikubwa Wilayani humo Mtaturu alisema kuwa serikali imekusudia
kuboresha kilimo na ufugaji ili viwe vya tija na kibiashara na kupelekea
kupunguza umasikini wa wananchi mwaka hadi mwaka.
Mtaturu anakuwa Mkuu wa Wilaya wa kwanza kukutana na kundi
la wazee Siku chache baada ya kuapishwa jambo ambalo halijawahi kutokea kwa
kiongozi mwingine yeyote Wilayani humo tangu Mkoa wa Singida ulipoanzishwa.
Kwa upande wao wazee hao wameonyesha wazi mapenzi yao ya
dhati kwa mkuu huyo wa Wilaya na kuahidi ushirikiano uliotukuka katika utendaji
wake.
Wakati huo huo wazee hao wamemshukuru Mh Rais Magufuli kwa
uteuzi alioufanya kumpeleka Mkuu huyo wa Wilaya kuongoza wananchi hao ambao
wameonyesha kukatishwa tamaa na baadhi ya viongozi wa serikali wilayani humo
ambao wameshindwa kutatua changamoto za wananchi.
Awali Dc Mtaturu alikuwa na kikao cha mapema na watumishi wa
Halmashauri na wakuu wa idara ili kukumbushana majukumu ya kila mmoja utendaji
wake na kuwasihi kufanya Kazi kwa bidii zaidi kwa kushirikiana na wananchi.
Mtaturu amewakumbusha watumishi hao wajibu wao wa kusimamia
miradi ya maendeleo kwa kupata thamani halisi ya fedha (Value for Money)
kushughulika na kero za wananchi ikiwemo kutafsiri ilani ya Uchaguzi kwa
vitendo ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewapa muda wa mwezi mmoja
watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wanaoishi Singida Mjini
takribani kilomita 41 kutoka Wilayani hapo wawe wamehamia Wilayani Ikungi kwani
amebaini ni watumishi wanne pekee ndio wanaoishi Wilayani hapa jambo ambalo
linapunguza ufanisi wa Kazi.
Katika sekta ya michezo Mtaturu alisema kuwa ili kuibua
vipaji na Mkoa wa Singida kwa muda mrefu umekuwa na Sifa ya kutoa wanariadha
hivyo ili kuenzi heshima hiyo anataraji kuanzisha Ikungi Marathon ili kuwapa
fursa Vijana wenye vipaji kuibuka na kufika mbali zaidi katika medani za
riadha.
No comments:
Post a Comment