Mohamed Mkonongo Mtaturu enzi za uhai wake
Asanteni sana kwa faraja zenu kwa msiba wa ghafla wa Mdogo wangu na rafiki yangu Mohamed Mkonongo Mtaturu nilipokea simu leo asubuhi muda wa saa 1:48 ya msamaria mwema akitumia simu ya marehemu akinijulisha amepata ajali daraja la salender akaniita nikamsaidie mdogo wangu, hakika alijua naweza kumsaidia kumbe msaada mkubwa upo kwa mungu aaah inaniuma sana pumzika kwa amani mdogo wangu katika umri wako wa miaka 43 umejitahidi sana kuisaidia jamii,
Alama zako za Upendo, juhudi, huruma kwa watu wenye mahitaji na kumjua mungu vitabakia kwenye mioyo yetu tuliokuwa nawe kwenye maisha ya hapa duniani na mungu atakulipa malipo mema inshaalah!Inaillah Wainaillah Rajiun,Amiin!katika majonzi yenye maombi kaka yako mpenzi na rafiki yako.
Miraji J. Mtaturu.
No comments:
Post a Comment