
Msanii nyota wa Bongo Fleva Nassib Abdul maarufu kama Diamond
Platnumz au SIMBA amefunguka juu ya ushiriki wa mama yake mzazi kwenye
video yake mpya ya Utaipenda.

Akizungumzia
suala hilo Diamond Platnumz (SIMBA) amesema hakutegemea kama mama yake
mzazi angekubali kushiriki katika video hiyo maana amekuwa akikataa hata
kuhojiwa na vyombo vya habari kutokana na kutokuwa huru akiwa mbele ya
kamera.

Diamond
ameeleza kufurahishwa kwake na mama yake kushiriki katika video yake ya
Utaipenda maana kusingekuwa na maana kama asingeshiriki kwasababu
amemtaja sana kwenye verse ya pili.
No comments:
Post a Comment