Sergio Aguero akimzidi Gary Cahill kuifungia City bao la kwanza |
MABINGWA
watetezi, Chelsea wamekiona cha moto kwa Manchester City baada ya
kuchapwa mabao 3-0 usiku wa leo Uwanja wa Etihad katika mchezo wa Ligi
Kuu ya England.
Sergio Aguero alianza kuifungia Manchester City dakika ya 32 katika mchezo ambao mshambuliaji
wa Chelsea, Diego Costa alidhibitiwa vikali wakati beki John Terry
alitolewa na kocha Jose Mourinho kwa mara ya kwanza baada ya mechi 177.
Nahodha wa City, Vincent Kompany akafunga bao la pili dakika ya 79, kabla ya Fernandinho kufunga la tatu dakika ya 85.
Kikosi
cha Manchester City kilikuwa; Manchester City: Hart, Sagna, Mangala,
Kompany, Kolarov, Toure, Fernandinho, Navas/Nasri dk65, Silva,
Sterling/Demichelis dk79 na Aguero/Bony dk83.
Chelsea;
Begovic, Ivanovic, Cahill, Terry/Zouma dk45, Azpilicueta,
Ramires/Cuadrado dk64, Matic, Willian/Falcao dk79, Fabregas, Hazard na
Diego Costa.
Wakati huo huo mara baada ya kichapo Chelsea imekubali kusajili beki wa kushoto wa kimataifa wa Ghana, Baba Rahman kutoka klabu ya Augsburg ya Ujerumani.
Baba Rahman (kulia) amejiunga na Chelsea kutoka Augsburg kwa Mkataba wa miaka mitano
Wakati huo huo mara baada ya kichapo Chelsea imekubali kusajili beki wa kushoto wa kimataifa wa Ghana, Baba Rahman kutoka klabu ya Augsburg ya Ujerumani.
Mabingwa
hao wa Ligi Kuu ya England ambao leo wamefungwa mabao 3-0 Manchester
City, wamesema watamsainisha Mkataba wa miaka mitano nyota huyo wa Ghana
kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 14.
Katika
dili hilo, beki huyo atapewa Pauni Milioni 3.5 zaidi katika posho
kulingana na kiwango chake Chelsea, Pauni 700,000 baada ya mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 21 kufikisha mechi 20 na nyingine Pauni Milioni
3.5 atakapofikisha mechi 100 — maana yake thamani yake inaweza kufika
Pauni Milioni 22.
No comments:
Post a Comment