TIMU
ya Arsenal imezinduka na kupata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya
England baada ya kuichapa mabao 2-1 Crystal Palace Uwanja wa Selhurst
Park jioni ya leo.
Mshambuliaji
Olivier Giroud alianza kuifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 16,
kabla ya beki wa kulia, Joel Ward kuisawazishia Palace dakika ya 28.
Beki
Damien Delaney akajifunga dakika ya 55 baada ya kazi nzuri ya Alexis
Sanchez kuipatia timu ya Arsene Wenger bao la pili la ushindi linalowapa
pointi tatu za kwanza msimu huu.
Kikosi
cha Crystal Palace kilikuwa; McCarthy, Ward, Dann, Delaney, Souare,
Cabaye, McArthur/Bamford dk80, Zaha/Chung-Yong dk76, Puncheon,
Bolasie/Mutch dk46 na Wickham.
Arsenal;
Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal,
Coquelin/Oxlade-Chamberlain dk64, Ramsey, Sanchez/Arteta dk75,
Ozil/Gibbs dk83, Cazorla na Giroud.
No comments:
Post a Comment