Monday, August 17, 2015

KINGUNGE ATEMWA CCM..



BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), limemvua ukamanda wa umoja huo mwanasiasa mkongwe na kada wa chama hicho Kingunge-Ngombale Mwilu.

Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda, alisema uamuzi huo umefikiwa juzi usiku, baada ya baraza kuu la umoja huo lilipokutana, pamoja na mambo mengine waliamua kumvua ukamanda Kingunge.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kikao cha baraza hilo, naye alitumia nafasi hiyo kuelezea nafasi ya vijana hao kuelekea uchaguzi mkuu, huku pia akiweka wazi kwamba, wanaoondoka CCM wanatoka kwa mapenzi yao wenyewe.

Kuhusu kuvuliwa ukamanda mkuu, Kingunge, Mapunda alisema “Baraza letu lilimvua ukamanda mkuu, Kingunge Ngombale Mwilu. Uamuzi huu ulitolewa kutokana na tabia na mwenendo wake wa hivi karibuni kwenda tofauti na maadili na taratibu za CCM.”

Aidha, kikao kimetoa mapendekezo kwa vikao vya Chama Cha Mapinduzi kuuangangalia upya uanachama wake na kuchukua hatua kubwa zaidi.

Mapunda alisema pia, baraza la umoja huo kupitia kikao chake cha juzi, kimeunda timu ya kampeni ambayo itafanya kazi na kamati ya utekelezaji kuhakikisha ushindi wa CCM kwa nafasi zote.

“Kikao kimemshukuru Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kwa hotuba nzuri ya ufunguzi wa baraza na kikao kimeahidi kutekeleza maagizo na maelekezo ya hotuba hiyo kwa matendo,” alisema.
Kingunge ni mmoja kati ya makada wa CCM ambaye alionesha hadharani kutoridhishwa na mchakato wa chama hicho katika kumpata mgombea urais kwa maelezo kuwa, taratibu zilikiukwa.

Kada huyo wa CCM wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia chama hicho, alikuwa upande wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye alikuwa akiwania nafasi hiyo ndani ya chama, lakini jina lake lilienguliwa.

Baada ya jina la Lowassa kuenguliwa, Kingunge hakusita kuelezea masikitiko yake dhidi ya chama chake, ambapo alisema tayari viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho walikuwa na wagombea wao mfuko na sehemu kubwa, utaribu wa kumpata mgombea urais wao si wa haki.

Rais Kikwete akizungumza na baraza hilo, alisema anayetoka CCM kwa sasa anatoka kwa hiari na mapenzi yake mwenyewe kwa sababu uamuzi wa nani agombee urais kupitia chama hicho ulifanyika kwa pamoja.

Aidha, Rais Kikwete alisema uamuzi huo ulifanyika kwa mujibu wa Katiba ya CCM na kuwa, ilipigwa kura ndani ya Halmashauri Kuu ya Taifa, baada ya mjadala mrefu, ambapo uamuzi ulichukuliwa kwa pamoja.

Pia, alisema hakuna haki iliyovunjwa katika mchakato wa kutafuta mgombea urais wa CCM, kwa sababu taratibu zote zinajulikana wazi na ni zile zile na ukweli ni kwamba, baadhi ya watu waliamua kutoka CCM, hata kabla ya vikao vya Dodoma kuanza.

Rais Kikwete aliwaambia vijana hao: “Aliyetoka, katoka mwenyewe kwa uamuzi wake mwenyewe, lakini pale tuliamua wote. Maana pale tulipokubaliana kupiga kura, tulikubaliana kupiga kura kwa majina yale matano, si uamuzi wangu pekee yangu, bali ulikuwa uamuzi wa sote. Maana tulijadiliana na kukubaliana kwa mujibu wa Katiba yetu, majina ni haya haya. Tukapiga na kura yakaisha.”

Alisisitiza :”Hivyo, anayetoka, anatoka kwa hiari yake mwenyewe kwa sababu pale Dodoma wote tulikubaliana, tuliamua wote kwa mujibu wa Katiba yetu na kwa kweli wote wanaotaka kutoka ndani ya CCM wanatoka kwa hiari yao wenyewe na wala si kwa sababu ya kunyimwa haki.”

Aliongeza, sasa mchakato umekwisha na aliyepata kapata na aliyesokosa kakosa. Mchakato huo haurudiwi tena na hawawezi kuitisha tena mkutano mkuu. Lililobaki sasa wanasubiri Dk.John Magufuli arudishe fomu na baada ya hapo ni Ihynae Ihyena na mambo yanakwenda.

” Haya ndiyo mapenzi ya Mungu. Katika mchakato huo wa Dodoma, CCM ilimteua Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli kuwa mgombea urais
ciao

No comments:

Post a Comment