Uboreshaji wa daftari hilo uliahirishwa kutokana
na kuchelewa kwa vifaa kutoka mikoani kwa ajili ya kuongezea ufanisi
kutokana na maeneo hayo kuwa na idadi kubwa ya watu wenye sifa ya
kuandikishwa.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), Julius Mallaba kwa vyombo vya habari, iliwataka
wananchi wote wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya
uandikishaji vitakavyokuwa kwenye vijiji, vitongoji na mitaa ili
kujiandikisha waweze kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Aliwataja wanaopaswa kuandikishwa ni watu wote
waliotimiza umri wa miaka 18 na kuendelea na wale watakaotimiza miaka 18
ifikapo Oktoba mwaka huu.
Wengine ni waliojiandikisha awali kwenye Daftari
la Kudumu la Wapigakura la zamani ili kuhuisha taarifa zao na kupatiwa
kadi mpya.
Mallaba aliwataja wengine wenye sifa ya
kujiandikisha kuwa ni wale wote wenye sifa lakini hawakuwahi
kujiandikisha kwenye daftari hilo.
Alisema wale wote wenye kadi za kupigia kura za
zamani wanatakiwa kwenda na kadi zao ili kurahisisha uchukuaji wa
taarifa zao na kadi hizo zitarudishwa NEC na watapata vitambulisho
vipya. Pia, wananchi wanatakiwa kujiandikisha katika vituo vilivyopo
ndani ya kata zao.
Mallaba aliwataka pia wananchi wa mikoa hiyo
kuhakikisha wanajiandikisha kwani bila kufanya hivyo hawataweza kupiga
kura wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kila siku kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa ifikapo saa 12:00 jioni.
No comments:
Post a Comment