Saturday, July 4, 2015
Jeshi la Syria laua wanamgambo 100 wa Daesh
Ndege za kijeshi za Syria zimefanya mashambulizi dhidi ya maeneo ya waasi katika mji wa Aleppo wa kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na kuua wanamgambo 100.
Vyombo vya habari vya eneo hilo vimeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wanamgambo hao wameuawa baada ya ndege za Syria kushambulia maficho kadhaa ya genge hilo la kigaidi.
Mashambulio hayo yamefanyika baada ya wanamgambo wa Daesh kushambulia kwa maroketi maeneo yaliyomo mikononi mwa serikali huko Aleppo siku ya Alkhamisi.
Raia wasiopungua wanne wameuawa na zaidi ya 70 kujeruhiwa katika mashambulio ya siku ya Alkhamisi ya wanamgambo hao.
Aleppo ni mkoa muhimu sana kiuchumi nchini Syria na baadhi ya maeneo ya mkoa huo yamo mikononi mwa genge la kigaidi la Daesh na kwamba jeshi la serikali linafanya juhudi za kukomboa maeneo yote yaliyobakia kutoka mikononi mwa kundi hilo la kitakfiri.
No comments:
Post a Comment