Thursday, July 23, 2015

MGOMBEA AMWAGACHOZI HADHARANI....

wagombea 12 wakiwa katika viti wakisubiri kuitwa mmoja mmoja ili kunadi sera zao kwa wajumbe wa ccm ngazi ya jimbo.

clala Mpambe wa Jesca Msambatavangu akiwa anazungumza na vyombo vya habari mara baada ya kupewa tuhuma za kuwapa madela akina mama na dada.

Na Denis Mkakala, Iringa



                Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa iringa ambaye ni mgombea wa ubunge kupitia  chama cha mapinduzi manispaa ya iringa ,hii leo amekumbwa na kashifa ya kutoa rushwa kwa wanachama wa chama hicho katika baadhi ya mikutano ambapo rushwa hizo zikiwa za Pesa tasirimu,madela aina ya magauni yenye nembo za bendera ya chama hicho pamoja na kuwanunulia pombe za kienyeji sawia na kuwashawishi wajumbe hao kutawanyika mara baada ya yeye kuzungumza.

Malalamiko hayo yakitolewa na wagombea kumi na mmoja ambao walikutana na waandishi wa habari na kueleza kuwa chama hicho kitakosa mgombea mwenyesifa wa kuwezakumuondoa mbunmge wa upinzani aliyeopo kwasasa kutokana na kiongozi huyo kufanya rafu ambayo inaweza kupelekea chama hicho kugawanyika katika hatua ya kuomba ridhaa kwa wajumbe wa chama hicho katika ngazi ya jimbo kabla ya kwenda kukatwa ngazi ya Taifa.

Kwaupande wake mtuhumiwa wa kashifa hiyo Jesca Msambatavangu amekanusha tuhuma hizo nakusema wagombea wenzie hao 11 kati ya wagombea 13 wote wamepanga njama hiyo ilikumuondoa kwakuwa dhali mapema upepo umeonyesha kuwa yeyendiye mshindi katika kura za maoni ambazo zinztarajiwa kupigwa tarehe 01 mwezi ujao.


No comments:

Post a Comment