Monday, July 20, 2015

David Kafulila aepewa tuzo ya mwanasiasa bora mwenye maono

Mbunge wa Kigoma kusini kwa tiketi ya NCCR mh David Kafulila amezidi kuujengea sifa Mkoa wa Kigoma na kuwa miongoni mwa wabunge na watu maarufu kutoka mkoani Kigoma kufanya vizuri kitaifa, awali sifa za mkoa huo maarufu kwa vipaji mbalimbali ilikuwa imeanza kutoweka kutokana na wanasiasa wanaotokea mkoani humo kutuhumiwa kuwa wasaliti na kuvuruga ustawi wa upinzani nchini kwa kudhaniwa wanatumiwa na chama tawala CCM ili kuudhofisha upinzani nchini.
Mh Kafulila ameyasema hayo leo jijini Dar-es-Salaam mara tu baada ya kupokea tuzo ya mwanasiasa bora mwenye maono,(kiongozi mwenye maono) Sambamba na Kafulila kupewa tuzo hiyo na taasisi ya Dream Success Enterprises.
Wengine waliopewa tuzo hiyo ni mwanahabari nguli wa habari za uchunguzi na habari za kina Said Kubenea pamoja na mwanahabari pekee mwanamke alionesha kupambana kwa vitendo dhidi ya vita ya mauaji ya Albino nchini bi Vicky Mtetema, huku Kubenea akipewa tuzo ya uwazi na ukweli.
Tuzo hiyo aliyepokea mh Kafulila imekuwa ya pili tangu mwaka huu uanze baada ya hapo awali kupokea tuzo nyingine kutokana na kuibua kashfa kubwa ya ufisadi wa Escrow na hivyo kuendelea kuung'arisha mkoa wa Kigoma.
Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa mwanasheria wa kwanza wa serikali ya Tanganyika Jaji Mark Bomani.
Akiongea na mwandishi wa habari hii mara tu baada ya kupokea tuzo hiyo, mh Kafulila alisema tuzo hii ni zawadi kwa wana-Uvinza mkoa mzima wa Kigoma na Watanzania kwa ujumla kwa kuendelea kumsapoti, bila kusahau wabunge wenzake wa upinzani kwa ushirikiano wanaompatia katika shughuli zake mbalimbali za kisiasa.

No comments:

Post a Comment