Wananchi wa jimbo la Iringa mjini wametoa maoni yao juu ya
Mbunge ajaye awe na vipaumbele gani huku kipaumbele cha uboreshwaji wa soko la
kihesa na barabara za maeneo mbalimbali za mjini hapa zikipewa kipaumbele zaidi hasa za uchochoroni ambazo kufikika imekuwa tatizo huku wakisema kuwa kuwapo karibu na zahanati ikiwa barabara hazifikiki kuweza kuwachukua wagonjwa hao linaweza kuwatatizo zaidi boara kungekuwa hakuna zahanati Alisema mama jenifa .
Nae Deo ambaye ni mkazi wa Mafifi
amesema Mbunge wa awamu hii anahitajika awe na vipaumbele vya kumkomboa
mwanamke hasa mjasiliamali anbaye anae jitafutia katika soko la chini kwa kuboreshewa
mazingira ya kufanyia biashara huku akitolea mfano wa soko la kihesa kuwa ni lamuda mrefu ingawa halijawahi kufanyiwa maboresho na kulifanya kuvutia watu wanaotoka maeneo mengine kutokimbilia soko la mkoa.
Aidha Raymond amemtaka Mbunge huyo kutatua tatizo la ajira
kwa vijana ambalo limekuwa sugu kwa muda mrefu sasa ikiwa kila kiongozi anayeomba lidhaa ya kuongoza hutumia vijana hao ili kupata madaraka ingawa tatizo hilo sasa ni lakimataifa anapaswa kutambua kwa ngazi yake anahitajika kutoa msaada zaidi .
Moja ya eneo la soko la kihesa Iringa |
No comments:
Post a Comment