Monday, June 5, 2023

Naibu Spika atembelea banda la Maonesho ya Ofisi ya Hakimiliki Tanzania - Katika Viwanja vya Bunge


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Musa  Azzan Zungu (Mb) akiwa ametembelea banda la Maonesho ya Ofisi ya Hakimiliki Tanzania - COSOTA leo Juni 05, 2023 katika Uwanja wa Bungeni Jijini Dodoma.

Maonesho haya ni kwa ajili ya kutoa elimu kwa Wabunge kuhusu majukumu yaliyo kwenye taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuelekea kusomwa kwa hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo ya mwaka 2023/2024.

No comments:

Post a Comment