Monday, June 5, 2023

JE,NI LINI SERIKALI ITAIPANDISHA HADHI BARABARA YA IRAMBO HADI NSONYANGA AMBAYO INAUNGANISHA BARABARA YA ISYONJE-MAKETE HADI NJOMBE TANZAM?"MBUNGE NJEZA"


Na Saida Issa,Dodoma

IMEELEZWA kuwa Tarehe 09 Januari, 2023, Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Njombe kilifanyika ambapo moja ya barabara zilizopendekezwa kupandishwa hadhi ni Barabara ya Irambo – Nsonyanga yenye urefu wa kilomita 22. 

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri TAMISEMI Deogratus Ndejembi alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza alipouliza Je, ni lini Serikali itaipandisha hadhi barabara ya Irambo hadi Nsonyanga ambayo inaunganisha barabara ya Isyonje – Makete hadi Njombe na Tanzam.

Mheshimiwa Spika, Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) naomba kujibu swali la Mheshimiwa Oran Manase Njeza, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, kama ifuatavyo:- Kamati ya Kitaifa ya Kupanga Barabara Katika Hadhi Stahiki (NRCC) ilifika Mkoani Mbeya tarehe 24 Februari 2023 na kutembelea barabara zilizoombwa kupandishwa hadhi ikiwemo barabara ya Irambo – Nsonyanga,"amesema.

Pia amesema kuwa Mapendekezo ya Kamati yamewasilishwa kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na yanachambuliwa na uchambuzi ukikamilika taarifa itatolewa. 

Endapo barabara hiyo itakidhi vigezo vya kupandishwa hadhi, itakuwa barabara ya Mkoa na itahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

No comments:

Post a Comment