Tuesday, May 2, 2023

Serikali Yakamilisha Usanifu wa Upanuzi wa miradi ya Maji Msalala


Na Saida Issa,Dodoma

SERIKALI imesema kuwa imekamilisha usanifu wa upanuzi wa miradi ya maji ya Mhangu-Ilogi na Nduku-Busangi itakayohudumia Kata za Ikunda, Mwakata, Menga, Shilela na Lunguya zilizopo Wilayani Msalala. 
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Maji Jumaa Aweso alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Msalala Iddi Kassim Iddi alipouliza:-Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka maji ya Ziwa Victoria katika Kata za Ikunda, Mwakata, Menga, Shilela na Lunguya Halmashauri ya Msalala.

"Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi Mbunge wa Msalala kama ifuatavyo:-Kwa sasa taratibu za kumpata Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi zinaendelea na ujenzi utaanza katika mwaka wa fedha 2023/24,"amesema. 

Mbunge Iddi alitaka kufahamu kuhusu mradi wa Nduku-busangi Ntobo kuwa ni mradi ambao umechukua muda mrefu sana na Kwa hatua iliyofikia kwa sasa wameseza kukosa kiasi Cha shilingi Milioni 50 kwaajili ya mkandarasi kuchimba mtalo na kuchelewa kwa mradi huo umesababisha sasa hospital ya wilaya ya Ntobo kukosa maji na kupelekea mlipuko wa magonjwa mbalimbali katika hopitali hiyo ya wilaya

Alitaka kujua kuwa ni lini Wizara itatoa kiasi hicho Cha fedha kwa dharura ili ipeleke fedha hizo na hospital ya wilaya iweze kupata maji pia alitaka kujua kuhusu Kata ya mwakata imepitiwa na Bomba kuu linalotoka kagongwa kwenda isaka na Kata hiyo Haina maji ni Nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba Kata hiyo inanufaika na maji hayo kwani Bomba hilo limepita katika maeneo hayo?

Akijibu maswali ya nyongezwa Waziri wa Maji amemhakikisha mbunge wa Msalala kuwa wizara ya maji mwezi huu imepokea Bilioni 67 kwaajili ya malipo ya wakandarasi.

"Kwaiyo moja ya maeneo ambayo tutawapa kipaumbele Cha haraka ni eneo Msalala kuhakikisha mradi huu unakamilika na wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama,

Eneo lapili Mheshimiwa Naibu spika ni juu ya mradi ambapo tunabomba kubwa linapita sera inasema Bomba kuu linapopita vijiji ambavyo vipo karibu na kilometa 12 kulia na kushoto mwa Bomba kuu ni lazima vipate huduma na nataka nikuhakikishie hili tumelipokea na tunakwenda kulifanyia kazi Kwa haraka,"amesema Aweso.

No comments:

Post a Comment