Tuesday, May 2, 2023

MBUNGE KATANI AIOMBA SERIKALI KUPELEKA FEDHA KUMALIZA UJENZI WA SEKONDARI KATA ZA MNCHIMBWE, KWANYAMA NA LITEHU


Na Saida Issa, Dodoma

SERIKALI inatambua jitihada zinazofanywa na wananchi katika kuibua miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule hivyo imeendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa kumalizia miradi hiyo.

Akijibu swali la Mbunge wa Tandahimba Katani Ahmed Katani Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Naibu Waziri Deogratus Ndejembi,lililouliza Je, lini Serikali itapeleka fedha kumalizia ujenzi wa Sekondari Kata za Mnchimbwe, Kwanyama na Litehu zilizojengwa na Wananchi.

"Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali la Mheshimiwa Katani Ahmed Katani, Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, mwaka wa fedha wa 2020/21, Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kupitia mapato ya ndani ilitoa shilingi milioni 200 kwa ajili ya umaliziaji wa Shule ya Sekondari ya Kwanyama,"amesema. 

Amesema kuwa Mwaka wa fedha wa 2021/22, Serikali illipeleka shilingi milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Litehu kupitia mradi wa SEQUIP na mwaka wa fedha 2022/23, shilingi milioni 250 zilitolewa na Serikali kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mndumbwe. Aidha, Shule za Sekondari katika Kata za Mnchimbwe, Kwanyama na Litehu zimekamilika, zimesajiliwa na tayari zinatumika. 

"Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha za umaliziaji wa maboma ya shule katika Halmashauri zote nchini kadri ya upatikanaji wa fedha,"amesema Naibu Waziri.

Kadhalika Mhe.Katani amehoji kuwa je,Serikali inaweza kuwapatia fedha kwaajili ya Ujenzi wa shule za Sekondari kwa Kata Serikali inatambua jitihada zinazofanywa na wananchi katika kuibua miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule.

Naibu Waziri amesema Kata hizo alizozitaja Mbunge Katani tayari Serikali tayari ipo mbioni kupeleka shilingi Milioni 470 kwenye halmashauri 184 Nchi nzima kwaajili ya Ujenzi wa shule zingine za Sekondari katika kata ambazo hazijapata shule za Sekondari.

No comments:

Post a Comment