Mamlaka ya Serikali mtandao Nchini (eGA) imepanga kuweka mwelekeo wa Serikali katika kuandaa na kutekeleza mikakati madhubuti lengo ikiwa ni Serikali kufikia uwezo wa kutumia teknolojia mpya zanazo ibuka hasa zile za akili bandia na sarafu za kidijitali na teknolojia za kifedha.
Taarifa hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa mamlaka ya serikali mtandao (eGA) Eng.Benedict Benny Ndomba wakati Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kikao kazi Cha Serikali mtandao kinachotarajia kufanyika februali 8-10 mwaka huu Jijini Arusha.
Alisema kuwa kuelekea kikao kazi Cha 3 Cha Serikali mtandao ambacho kinatarajia kufanyika Jijini Arusha mamlaka hiyo imejipanga kuandaa na kutekeleza sehemu moja ambayo huduma ya Mitandao zote zinakua zinapatika kwa urahisi.
Kuelekea kikao kazi hicho alisema lengo kubwa ni kuwakutanisha wadau mbalimbali wa Serikali Mitandao Ili kujadiliana juu ya mafanikio ,changamoto pamoja na kuweka mikakati mbalimbali ya kukuza Serikali mtandao matumizi sahihi na salama ya TEHAMA katika Taasisi za Umma.
"Mamlaka ya serikali mtandao eGA ndiyo taasisi iliyopewa jukumu la kuratibu ,kusimamia na kukuza juhudi za Serikali mtandao pamoja na kuhimiza uzingatiaji wa sera,sheria , kanuni,na viwango vya miongozo ya serikali mtandao katika Taasisi za Umma Ili kuhakikisha matumizi sahihi na salama ya TEHAMA yanazingatiwa katika Taasisi hiyo," alisema Mkurugenzi huyo.
Aidha alieleza mafanikio yatokanayo na mamlaka ya serikali mtandao ikiwa ni pamoja na kusimamia uzingatiaji wa sera,sheria na miongozo ya serikali mtandao kwa taasisi za umma ,kuwezesha usanifu na Ujenzi wa mifumo ya Serikali mtandao ya kitaasisi na ya kisekta Ili kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.
"Ndugu wanahabari pia taasisi ya serikali mtandao imepata mafanikio katika kuboresha na kuongeza maswala ya kusimamia uendeshaji wa miundombinu shirikishi ya serikali mtandao kwa kutoa msaada wa kiufundi kwa taasisi za umma katika matumizi sahihi na salama ya huduma za Serikali mtandao katika kuwahudumia wananchi"alisema.
Mamlaka ya serikali mtandao eGA inatarajia kupokea wadau elfu moja (1000) kutoka katika mashirika na Taasisi za Umma wakiwemo maafisa Masuhuli ,wajumbe wa Bodi ,wakuu wa vitengo vya TEHAMA maafisa TEHAMA,maafisa Rasilimali watu,Maafisa mipango ,maafisa Mawasiliano,wahasibu pamoja na watumishi wote wa mifumo ya TEHAMA Serikali hao wote wanatarajia kushiriki kikao kazi kitakachofanyika kuanzia February 8-10 Jijini Arusha.
Katika kikao kazi Cha Serikali mtandao kitaongozwa na Kauli mbiu isemayo "mifumo Jumuishi ya TEHAMA kwa utoaji wa huduma Bora kwa umma" huku falsafa ya kauli mbiu hiyo ikiwa ni kuhamasisha Taasisi za Umma kutumia mifumo Jumuishi inayowasiliana katika utendaji kazi kuanzia mwanzo Hadi mwisho.
No comments:
Post a Comment