Tuesday, February 28, 2023

WATEJA 6,752 WAFUNGIWA MITA ZA MAJI ZA MALIPO KABLA IRINGA


Na Saida Issa,Dodoma

MAMLAKA ya Maji safi na usafi wa mazingira Iringa (IRUWASA) imesema kuwa imefanikiwa kuwafungia wateja 6,752 mita za maji za malipo kabla (prepaid Water Meters) na kuwa mamlaka hiyo inaongoza kwa kufunga mita za maji nyingi za malipo kabla.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi David Pallangyo,wakati akielezea Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo leo Februari 27,2023 jijini Dodoma.

Mhandisi Pallangyo amesema kuwa kufungwa kwa mita hizo imesaidia kupunguza malalamiko kutoka kwa wanachi na imesaidia pia kuondoa ule urundikaji wa madeni ya maji.

"Kupitia mfumo huo wa Malipo Kabla IRUWASA imefanikiwa kupunguza kiasi cha maji yasiyolipiwa kwa upande wa Iringa mjini kutoka wastani wa asilimia 24.6 mwaka 2020 hadi wastani wa asilimia 22.52 kwa mwezi Disemba 2022," amesema.

Pia Mhandisi Palangyo amesema kuwa idadi ya wateja waliounganishwa na majisafi imeongezeka kutoka 28,133 mwaka 2020 hadi 40,549 kwa mwezi Disemba 2022.

Aidha amesema zipo changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo ni uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji ,kutokana na shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika vyanzo hivyo kama vile kilimo,ufyatuaji wa matofali,ufugaji,uchimbaji wa michanga pamoja na ukataji wa miti,ambavyo vimekuwa vikipelekea kupungua kwa maji katika kina cha mto Ruaha mdogo hasa katika kipindi cha kiangazi.

Amesema uchafunzi na uharibifu wa vyanzo vya maji vimekuwa ni tatizo licha ya elimu inayoendelea kutolewa kwa jamii lakini bado tatizo hili limeendelea kushamili.

"Niwaombe waandishi wa habari mtumie kalmu zenu vizuri kupanda na uharibifu huu wa vyanzo vya maji kwani tunatambua nyinyi mna uwezo huo na nguvu ya kuishawishi jamii kuachana na vitendo hivi,"amesema Mhandisi Pallangyo

Na kuongeza "Changamoto nyingine ni uwepo wa mtandoa wa maji taka usiyokidhi mahitaji ambapo mfumo uliopo wa kukusanyia na kusafirishia majitaka umewafikia kwa asilimia 6.8 ya wakazi wa Iringa Mjini, wakati katika miji ya Kilolo na Ilula mfumo huo haupo kabisa,"Amesema .

MIPANGO YA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA MAJISAFI NA UONDOSHAJI MAJITAKA MANISPAA YA IRINGA NA MIJI YA KILOLO NA ILULA

Miradi iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na Mradi wa kuboresha huduma ya maji maeneo ya pembezoni ambapo mnamo mwezi Desemba, 2022, IRUWASA ilikamilisha utekelezaji mradi wa kusambaza maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa mji wa Iringa yaliyo kwenye kata za Mseke, Kalenga na Kiwele. 

Amesema Mbali ya wananchi wapatao 12,930 wanaonufaika na mradi huu, Taasisi mbalimbali kama vile shule, hospitali, vyuo na maeneo ya biashara zitanufaika pia.

Amesema Gharama za mradi huu ni Tshs 1,818,726,402 ambapo IRUWASA iligharamia Tsh. 751,140,000 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato na 1,067,586,402 ni mkopo kutoka benki ya TIB. 

"Mradi huu utakapokamilika utaleta manufaa kwani huduma ya maji kwa miji ya Iringa, Kilolo na Ilula itafikia 100%
Upatikanaji wa majisafi na salama utakuwa saa 24, siku saba (7)
Jumla ya wananchi 456,010 watanufaika na huduma ya majisafi hadi mwaka 2045," Amesema 

Mwisho

No comments:

Post a Comment