Na Saida Issa, Dodoma
IDDY Kassim Iddy Mbunge wa Msalala amesema wamejipanga vizuri kukabiliana na hoja zote zitakazoibuka kutoka kwa vyama vya upinzani.
Mbunge huyo amesema hayo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma alipokuwa akielezea maono na maamuzi ya Rais Samia kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa nchini.
Alisema kuwa kazi kubwa wameifanya kwa kipindi kifupi na bado wanaendelea kutekeleza ahadi za CCM chini ya serikali ya awamu ya 6 ambayo ni Serikali ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Alisema mambo mengi yamefanyika katika maeneo yao na hivyo Kutokana na ajenda zilizokuwepo kutoka kwa upinzani tayari wamekwisha kuzijibu kwa kutatua changamoto za wananchi.
"Ukija katika Jimbo langu la msalala utaona kuna zahanati zaidi ya 34 tumemaliza kwa mkupuo,kunavituo vya afya zaidi ya 4,tunashule mpya 2 ambazo tumezijenga kuanzia chini,tunajenga Chuo Cha veta,tunajenga Chuo Cha wauguzi zaidi tunabarabara inayotoka kakola mpaka kahama ambayo imeghalimu kiasi Cha shilingi Milioni 40,
Utaona katika miundombinu kama barabara kunafedha nyingi zimekuja na mabarabara mengi tumeyafungua na Leo utaona Kata nyingi ambazo zilikuwa hazifiki saizi zinafikika bila changamoto,"alisema
Alisema kuwa hawanakazi ya kujibu Hoja Kutokana na Yale waliyoyafanya katika maeneo yao hasa kuleta maendeleo kwa wananchi katika Kila nyanja ikiwemo miundombinu kuboresha.
Changamoto haziwezi kukosekana hata nyumbani kwako huwezi maliza changamoto zote lakini kwa kiasi kikubwa tumetekeleza ilani ya chama Kwa Yale tuliyokuwa tumeyaahidi kwa wananchi,
Wananchi wangu nawasihi watulie tu sisi viongozi wao tumejipanga kuleta maendeleo kupitia Chama Cha Mapinduzi,"alisema Iddy.
No comments:
Post a Comment