Afisa elimu Mkoa wa Singida Maria Lyimo akizungumza kwenye mkutano wa uhamasishaji programu ya serikali ya Shule bora hapo jana. |
Mkutano ukiendelea |
PROGRAM ya Serikali ya Tanzania chini ya ufadhili wa
serikali ya Uingereza inayotekelezwa katika mikoa 9 ikiwa na lengo la kuinua ubora
wa elimu ya awali na msingi ijulikanayo kwa jina la SHULE BORA imewahimiza Wawakilishi,Wasimamizi
na wahariri wa vyombo vya habari Mkoa wa Singida kushiriki kikamilifu katika
program hiyo kwa kuandika na kuripoti changamoto na vikwazo vinavyowakwamisha
watoto kushindwa kupata elimu bora hapa nchini.
Akizungumzia Programu hiyo kwenye Mkutano wa uhamasishaji wa programu
ya shule bora kwa wasimamizi na wahariri wa vyombo vya habari mkoani hapa
Raymond Kanyambo amesema shule bora
inabaini changamoto zinazokwamisha ujifunzaji na ufundishaji wa watoto elimu ya
awali na msingi na kuzitafutia ufumbuzi ili kila mtoto wa kitanzania anapata
elimu bora .
Kanyambo amesema kwenye program hiyo kundi la
waandishi wa Habari litakuwa msaada mkubwa endapo litashirikiana na shule bora kuzibaini changamoto hizo zinazokwamisha ujifunzaji na ufundishaji wa watoto shuleni hivyo akatoa wito
kwa wandishi wa Habari Kuwajibika katika suala hilo.
“Tunategemea
mshiriki katika programu hii kuzibaini baadhi ya changamoto zinazopelekea
watoto wasisome ama wasipate elimu bora na kisha itafutwe njia ya kuondoa
changamoto hiyo, kama waandishi mnahaki ya kuhoji hali ya uandikishaji wa
wanafunzi wangapi wameripoti, wangapi wamefaulu, je kundi wenye ulemavu lipo
vipi kitaluuma?, hivyo mshirikiane na sisi katika kuinua elimu kwa watoto wetu ” Alisema Kanyambo.
Afisa Habari Mkoa wa Singida Bashir Juma (Kulia) na Mwandishi wa habari Imani Musigwa( Kushoto) Wakiandika mambo muhimu kwenye Mkutano huo. |
Kaimu Afisa Habari Halmashauri ya Itigi Bw. Luganuzi akichangia mada ya ushirikishwaji wa wandishi wa habari mkoani Singida . |
Meneja wa Mawasiliano wa Shule Bora Raymond Kanyambo akiwasilisha mambo mbalimbali kwenye mkutano huo. |
Ameongeza kwa kutaja malengo ya shule bora kuwa ni pamoja na kuboresha Ujifunzaji wa watoto wote shuleni kuhakikisha watoto wote wanaenda shule na kusoma, Kuboresha Ufundishaji wa walimu ili wawasaidie watoto kupata elimu bora , Ujumwishaji wa watoto wote shuleni kuhakikisha wanapata elimu bora katika mazingira salama na wezeshi huku lengo lingine akitaja kuwa ni kuimarisha mifumo ya usimamiaji elimu ambapo kundi lililolengwa ni la wasimamizi wa ubora wa elimu wakiemo viongozi wa halmashauri na wadhibiti ubora.
Awali
akifungua Mkutano huyo wa shule bora na waandishi wa habari Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Mwalimu Dorothy
Mwaluko,aliwataka wasimamizi wa program ya wa Shule Bora inayotekelezwa katika mikoa tisa
nchini kutengeneza mfumo wa kutoa mafunzo kwa walimu wa Mkoa wa Singida ili
kuinua viwango cha elimu mkoani humo
"Msiwe
na kituo cha mafunzo sehemu moja, Mnatakiwa kuwa na vituo walau Kila
halmashauri kuwe na 'trainers' Pamoja na Vituo vya kufanyia Mafunzo na kuwakutanisha
walimu wengi ili wote waguswe kwa wakati mmoja"
amesema
Mwl. Mwaluko alitumia nafasi hiyo kuwasistiza waandishi wa Mkoa wa Singida katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwake ,kuandika habari za kutanga vivutio vilivyopo ndani ya mkoa pamoja na zile zitakazo saidia kutatua changamoto kwenye jamii kuliko zitachochea mifarakano na kurudisha nyuma Maendeleo ya wananchi
Mratibu wa Program hiyo Mkoa wa Singida, Samwel
Daniel alisema program hiyo inawahusu wanafunzi wa shule za awali na msingi na
kuwa walitoa mafunzo endelevu kwa walimu wakuu, mahiri na taaluma ambapo walimu
1774 wamenufaika nayo.
Programu ya Shule Bora imefadhiliwa na Uingereza kwa Paundi
milioni 89 ambazo ni sawa na Bilioni 271 za kitanzania, ambazo zitatumika
kwaajili ya uinua ubora wa elimu kwenye mikoa yote 9 ili kuhakikisha watoto
wote hata wale wenye changamoto mbalimbali wanapata fursa ya kusoma.
Washiriki wa Mkutano huyo ulioandaliwa na shule bora kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza wakiwa kwenye picha ya Pamoja baada ya ufunguzi kufanyika. |
No comments:
Post a Comment