Na Mathias Canal,
WEST-Dar es salaam
Timu ya watu watano imeanza kazi rasmi leo tarehe 5 Septemba
2022 ya kufuatilia utoaji mikopo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka
2017/2018 hadi mwaka 2021/2022.
Timu hiyo itakayofanya kazi ndani ya mwezi mmoja itaongozwa na Prof
Allan Mushi ambaye ni mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, na
wajumbe wake ambao ni Idd Makame kutoka Zanzibar na Dkt Martin Chegeni ambao
wote kwa pamoja ni wataalamu wa mifumo waliobobea katika sayansi ya Kompyuta na
Takwimu.
Akitangaza kuanza kazi kwa timu hiyo Jijini Dar es salaam katika
ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu-HESLB wakati wa kikao kazi
cha Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya HESLB, Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda amesema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa
malalamiko yanayotolewa kuhusu Bodi ya Mikopo yanapatiwa ufumbuzi.
Waziri Mkenda amesema kuwa serikali inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan imeongeza Bajeti hadi
kufikia Bilioni 570 za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu hivyo ni lazima
kuwe na usimamizi wa uangalizi wa hali ya juu.
“Hatufanyi hivi kwa sababu ya kuumbuana ila ni kwa sababu ya
kutaka uwazi na uwajibikaji na kwa sababu hiyo ni lazima kutoa mikopo kwa haki
na vigezo stahiki vilivyowekwa na serikali bila kujuana” Amekaririwa Waziri
Mkenda
"Shunguli za elimu zinahitajika kwa kila mtu hivyo ni
wajibu wetu kufanya kwa haki na uwajibikaji uliotukuka, hatutatoa mikopo kwa
kujuana kwa undugu, urafiki, au ujamaa hakuna (Robbing), tunataka haki"
“Na kwenye hili tunakaribisha watu watoe taarifa kwa sababu kama
kuna mtoto wa Mkenda uliyesoma nae utakuwa unamjua baba yake ni nani na uwezo
wake, halafu wewe unaona mtu huyo amepewa mkopo toa taarifa” Amesisitiza Waziri
Mkenda na kuongeza kuwa
Prof Mkenda amesema kuwa Mtu yeyote ambaye ana wasiwasi na
utoaji wa mikopo anakaribishwa ili aweze kuisaidia timu kufanya kazi yake kwa
kuwa na taarifa zenye usahihi wa hali ya juu kutoka kwa wanachi husika.
MWISHO
No comments:
Post a Comment