KATIKA kipindi cha
mwaka 2020 hadi 2022, kumekuwepo makubaliano ya kisera ya kukomesha ukatili
dhidi ya kuku na kitiwa saini zaidi ya mashirika 500 duniani ambapo Bara la
Afrika yapo mashirika 15 ambayo yamekubali ukomeshaji wa ukatili dhidi ya kuku.
Aidha, zaidi ya
mashirika 2,300 ya chakula dunia yamepitisha sera za ustawi wa kuku ambazo
huondoa vizimba vinavyotumika kufuga kuku wanaotaga mayai ambapo kampuni 982
zimekamilisha kwa ufanisi ufugaji kuku wa mayai matumizi ya vizimba vya betri.
Hadi kufikia Aprili
2022, asilimia 88 ya kampuni zilizotoa ahadi ya matumizi ya mayai ambayo
hutagwa na kwa kutumia ufugaji huria wa kuku, zimetimizwa matakwa hayo.
Ili kuhakikisha
mkakati huo unafikiwa, Mei 16, 2022 Shirika linalotetea haki za wanyama Open
Wing Alliance (OWA) ilizindua ripoti ya ufugaji huru ya mwaka 2022.
Ripoti hiyo ya pili
iligusia uzalishaji mayai yatokanayo na ufugaji huria wa kuku ambapo ripoti
hiyo inatoa fursa kwa kila kundi na umma kuelewa kwamba kampuni nyingi
zinatimiza ahadi zao za ustawi wa wanyama, lakini kuna baadhi ya kampuni ambazo
zinarudi nyuma linapokuja suala la maendeleo, uwazi katika haki za wanyama.
Muungano wa The Open
Wing Alliance duniani, umekuwa ukifanya kazi bila kuchoka kuhakikisha
kunakomeshwa matumizi ya kikatili ya kuwafungia kuku wanaotaga mayai kisha
kuingizwa katika mfumo wa chakula hasa viwandani.
Muungano huo
unahusisha zaidi ya mashirika 80 kutoka nchi 63 ambayo yamekuwa yakifanya kazi
kwa zaidi ya muongo mmoja ili kupata ahadi ya kukomesha ukatili dhidi ya kuku
kutoka kwa kampuni kubwa zaidi za chakula duniani.
Tanzania nayo haiko
nyuma katika mapambano dhidi ya ukatili wa wanyama, kwani OWA imekuwa
ikishirikiana na mashirika mbalimbali ya ustawi wa wanyama.
Miongoni mwa mashirika
hayo ni shirika la Education for African Animals Welfare (EAAW) katika
kutekeleza shughuli zake hususan utoaji wa elimu na kampeni zinazolenga
kukomesha ukatili dhidi ya wanyama hasa kuku waliofungiwa kwenye vizimba.
Akizungumzia mkakati
wa kutokomeza ukatili dhidi ya kuku, Mkurugenzi wa OWA, Alexandria Beck,
anasema kuendelea kupata ahadi nyingi katika kutekeleza sera ya ustawi wa
wanyama, ni kiashirio muhimu cha maendeleo kwa wanyama wanaofugwa kwa ajili ya
chakula.
“Ingawa tunajua kwamba
ahadi pekee hazitasababisha kuboreshwa kwa hali za wanyama. Ili kuwaokoa kuku
kutokana na maisha ya ukatili ya kufungiwa kwenye vizimba vya chuma, tunahitaji
kuona kampuni zinatengeneza na kutoa taarifa kuhusu maendeleo kuelekea malengo
yao ya ufugaji huria,” anaeleza.
Beck anasema takwimu
zinaonyesha kwamba siku zijazo hakutakuwa na ufugaji wa vizimba na zaidi ya
asilimia 11 ya kuku duniani, hawafugwi katika vizimba.
Yapo baadhi ya
mashirika ambayo yana sera ya kuondoa matumizi ya vizimba katika kufikia
asilimia 100 ya mayai yatokanayo na kuku wasiofugwa kwenye vizimba, bado
hawajaweka wazi hadharani maendeleo yao ya hatua iliyofikiwa katika maeneo yao.
Miongoni mwa kampuni
hizo ni Hilton Hotels, Radisson Hotels Group na Unilever. Hata hivyo, barani
Afrika kuna mashirika yaliyofikia na kutimiza ahadi ya uondoaji vizimba katika
ufugaji wa kuku, ambayo ni Danone, Marriott, Starbucks na Kraft Heinz ambayo
yanaripoti kwa uwazi hatua zilizofikiwa.
Mapema mwaka huu,
kampuni ya kimataifa ya Majid Al Futtaim ambao ni wauzaji wakubwa wa mazao ya
kuku kupitia maduka ya Carrefour nchini Kenya, Kameruni, Uganda na Misri
walitoa ahadi ya kutekeleza sera ya kimataifa yakutofungamana na wauzaji mayai
ya kuku wanaofugwa katika vizimba.
Majid Al Futtaim
ilionyesga namna ambavyo watumiaji wa mayai wanavyojali ustawi wa wanyama. Hata
hivyo bado kuna changamoto kwa ustawi wa kuku katika ukanda wa Afrika, kwani
zipo kampuni zimekuwa zikisuasua kukubaliana na sera ya uondoaji vizimba kwa
kuku wa mayai wanaofugwa.
Pia, wauzaji wa mayai kwa reja reja kama vile Pick n Pay, Shoprite na Massmart, wanahitaji kujitolea zaidi kwa kusisitiza ufugaji kuku bila vizimba ili kudhihirisha kwa umma kwamba wanajali ustawi wa wanyama hususan kuku.
No comments:
Post a Comment